Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ili kushinda umeya kati ya ccm au chadema waingie mkataba na mh michael kivuyo yeye awe kaimu meya ili kupata kura yake
is this legal?Jamani usanii mwingine ni mbaya sana. Mkurugenzi wa jiji aliwatangazia madiwani wote wakiwamo wa CCM kwamba kuna semina baada ya kutokubaliana kuhusu mamluki kutoka Tanga lakini baadae CCM wao wakaitana baadae Chadema wakshangaa kuwa wako peke yao ktk semina, wakakimbilia Manispaa wakakuta CCM wenzao na yule wa TLP wameshafanya uchaguzi na kujipa umeya na kumpa wa TLP Unaibu
is this legal?
is this legal?
kabisa . ukijumlisha wajumbe wa ccm na huyo wa tlp tayari wanapata zaidi ya 50% kwahiyo huyo meya ni wa halali kabisa kisheria
Jana tulionya kuhusu watu madiwani wa CHADEMA kutokujihusisha na kitendo chochote kitakachoruhusu uchaguzi ufanyike bila wao kuwepo. Uchaguzi sasa umefanyika na CCM wamechukua Halmashauri na hiyo imetoka.
Diwani wa TLP tayari sasa keshapata unaibu meya.
Narudia tena nilosema jana, CCM wanapotaka kitu na wewe ukaweka mizengwe, ama watakuhamisha, au watakuundia kesi ulale ndani wafanye wanavyotaka au watakutuma usafiri nje ya nchi au watakulaza hospitali kwa nguvu hata kama huumwi ila wapitishe wanachotaka. Nia ya CCM ilikuwa ni kuhakikisha walau madiwani wawili wa CHADEMA hawaingii kwa kikao na hilo wamefanikiwa.
CHADEMA mnapoona kuwa mnaelekea kushinda, mjitahidi sana kutokuwa na hasira. Muepuke kumshikia manati kuku wenu kwani wapita njia wanaweza wakapiga mayowe wakifikiri ni vibaka. Kila jambo lifanyiwe uchunguzi wa kina. Epukeni kumkimbiza kichaa alowanyanganya taulo. CCM inajifanya kichaa ili uikimbize watu wakushangae wakati yenyewe inakamilisha mambo yao. Ukirudi wameshamwaga maji yako na sabuni wamechukua.