Mindyou
JF-Expert Member
- Sep 2, 2024
- 1,869
- 4,877
Wakuu,
Huyu Mbunge wa COVID 19 ameamua kwenda jino kwa jino na Lissu huko Singida Mashariki
==============================================
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Nusrat Hanje, ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Akitangaza azma yake Februari 20, 2025, nyumbani kwake Ikungi, Singida, wakati wa Maombi na Dua ya Kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Hanje amesema ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Singida Mashariki.
Ameeleza kuwa nia yake ya kugombea inatokana na hamu ya kuwasaidia wananchi, huku akisisitiza kuwa ubunge wake hautakuwa kwa ajili ya kujitajirisha.
"Nafikiri mtapata Mbunge ambaye kwa mara ya kwanza mtafurahia kuwa naye, kwa sababu sijapanga kutajirika kupitia Ubunge. Nitahakikisha ninagawana nanyi kadri inavyofaa," amesema Hanje.