Pre GE2025 Mbunge wa Covid 19, Nusrat Hanje atangaza kugombea jimbo la zamani la Tundu Lissu, Singida Mashariki

Pre GE2025 Mbunge wa Covid 19, Nusrat Hanje atangaza kugombea jimbo la zamani la Tundu Lissu, Singida Mashariki

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Hajataja chama

..huo ndio mtihani.

..kiti cha ubunge lazima kibaki CCM.

..Je, CCM watampitisha?

..huenda anataka aende kwenye kura ya maoni ya CCM, ashindwe, halafu Mama Abduli amkumbuke ktk teuzi nyingine.
 
Covid 19 , kama sio wao vibaraka wao na wanaharam wenda ndo wameanzisha andiko hili.

OK Nyie Covid 19 why zalilisha nchi achana na chama cha awali kabla ya kufukuzwa?

Covid 19 ni majangili kwa lugha nyepesi ,ila ila tukitumimia lugha ngumu ni wezi wa taifa , hivi waweza kuwa binadam wa kawaida tu , watu wanakunyoshea vidole kwa miaka mitano kwamba wewe ni mwizi wa Taifa na bado ngangania kaa Bungeni ? Alafu ati leo wajivalisha nguo za ccm ,kwamba wanaccm hawakuoni kwamba hu tapeli japo na uchawa uliowajaa? Sio mda nyie viumbe mtazitapika asema Bwana,pumbavu
 
Wakuu,

Huyu Mbunge wa COVID 19 ameamua kwenda jino kwa jino na Lissu huko Singida Mashariki

==============================================

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Nusrat Hanje, ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akitangaza azma yake Februari 20, 2025, nyumbani kwake Ikungi, Singida, wakati wa Maombi na Dua ya Kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Hanje amesema ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Singida Mashariki.

Ameeleza kuwa nia yake ya kugombea inatokana na hamu ya kuwasaidia wananchi, huku akisisitiza kuwa ubunge wake hautakuwa kwa ajili ya kujitajirisha.

"Nafikiri mtapata Mbunge ambaye kwa mara ya kwanza mtafurahia kuwa naye, kwa sababu sijapanga kutajirika kupitia Ubunge. Nitahakikisha ninagawana nanyi kadri inavyofaa," amesema Hanje.

Com wanamuogopa Lissu mpaka wanafanya mambo ya kitoto mno
 
C
Sio uchaguzi wa mwaka huu bro...😀😀... trust me and sticky this comment, hakuna rais wala makamu wa rais atakayembeba mtu yeyote katika uchaguzi wa kipindi hiki... wote hao wako bize kupambania nafasi zao maana mpaka muda huu zipo 50/50... Halafu ndio useme wambebe huyo Nusura.... No way... Uchaguzi wa mwaka ni wa kihistoria na wa tofauti kuliko yote... Kama Chadema wangekua na vision ya mbali wangeachana na hayo marekebisho waingie hivi hivi, niamini hakuna kura ingeibiwa au polisi kuingilia.
Kipi kinakufanya uamini hayo?
 
Limekuwa limshangazi aisee. Kweli pesa sabuni ya roho.
 
Mkuu siku hizi naona kichwa chako kimepoteza focus kabisa. Chuki iliyonayo kwa Lissu inakufanya hata uone ni bora Samia ateue wabunge wote wa Tanzania kuliko Lissu kupata tena ubunge. Hili jambo huwa linanishangaza sana. Watu wengi walio upinzani wanapotofautiana na wenzao wanakuwa wabaya kuliko hata CCM.
Kwahiyo unataka niandike unachopenda kusoma? Acheni mentality Za kipumbavu na kitoto!! Kwani Nusrat Hanje Hana haki Za kidemokrasia Za kuchagua na kuchaguliwa?

Ni dhambi mtu akisema atagombea? Ulitaka nisemeje ili ufurahi? Hizi akili Za kihayawani ndo mnataka tuzikubali?

Narudia Tena Nusrat ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika chaguzi kama mtanzania yeyote mwenye sifa…. You can take it to the nearest bank!
 
Mtaturu ana wakati mgumu jimboni kwake kama huyu dada atagombea kwa tiketi ya CCM
 
Unajua Tanzania tuna hasara kubwa sana ambayo athari zake zitajitokeza miaka ijayo na kila mtu atatucheka. Kwenye uchaguzi rais ndiye anaamua nani ashinde na siyo wananchi. Ndiyo hawa hawaogopi wananchi.
Hii ni kweli kabisa .

Ndio maana hata polisi wamekua ni tawi la CCM kupigania waliowapa vyeo vya juu washinde .
Wanashindwa kabisa kujua kuwa chama chochote kikishinda kina wajibu wa kuongoza nchi na kumata amiri jeshi mkuu .

Yaani Mfano wananchi wakimchagua Lisu kuwa Rais askari wa chini bado watabaki na wajibu wao na majukumu yao . Hofu ni wale wa juu ambao wengi ni Makada wa Chama tawala na ndio mara nyingi wanatumika kuuliza na kutoa amri za kuua watu.
Hawa wanahofu ya kuondolewa kwenye nafasi zao kutokana na vitendo vyao vya kupendelea chama kimoja na kufumbia macho uhalifu wakati wa uchaguzi unaofanywa na UVCCM .
 
NUSRAT HENJE.

Ni mwanachama wa CCM.
Ni mke wa Maulid Kitenge.

Dada anatamaa kubwa sana ya madaraka.
 
Sio uchaguzi wa mwaka huu bro...😀😀... trust me and sticky this comment, hakuna rais wala makamu wa rais atakayembeba mtu yeyote katika uchaguzi wa kipindi hiki... wote hao wako bize kupambania nafasi zao maana mpaka muda huu zipo 50/50... Halafu ndio useme wambebe huyo Nusura.... No way... Uchaguzi wa mwaka ni wa kihistoria na wa tofauti kuliko yote... Kama Chadema wangekua na vision ya mbali wangeachana na hayo marekebisho waingie hivi hivi, niamini hakuna kura ingeibiwa au polisi kuingilia.
Mkuu umeandika vizuri ,ila tumechoka, vijana wetu kua vilema ,uliwa , binafsi ni mwana chadema ila sina shida kabisa akishinda mwana ccm kwa njia ya haki , awe mbunge, diwani ,au Rais , hii tabia ya kutumia watu huwa wenzao ,tia virema wenzao haikubaliki naunga mkono msimamo wa chama cha chadema .

Na kwa hili chama chochote kikasimama kwa hili nipo nacho mguu sawa
 
Maandiko yako nilipoyasoma nilimaizi kiwango chako kikubwa cha upumbavu mkuu wangu.....

Si kosa langu ,nasahihishaje upumbavu wako ulio sentimeta chache kutoka kidevuni mwako ?!!
Alafu unakaa viti virefu na kujisifu your tank think ya ccm au wa mama , hopeless kabisa.

Hiko hivi covid 19 wataisikia chadema kama mbigu na Dunina, na yeyote atakae jaribu kuwaleta / warudisha chadema atakufa mdomo wazi , asema Bwana.

Vyama viko vingi waende huko , wajeeuhi chama ,kama sio kukidhalilisha chama period.

Ccm ,Ndugai alipo amusha mdomo alichofanyiwa Mungu anajua, leo mwanaccm amepinga uteuzi wa Mgombea kavuliwa uanachama , hii ccm ya leo vipi? Michawa ipo shangilia tu .

Hiko hivi ccm mtashindana ila hamtashinda ,asema Bwana
 
Wakuu,

Huyu Mbunge wa COVID 19 ameamua kwenda jino kwa jino na Lissu huko Singida Mashariki

==============================================

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Singida, Mhe. Nusrat Hanje, ametangaza nia ya kugombea Ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Akitangaza azma yake Februari 20, 2025, nyumbani kwake Ikungi, Singida, wakati wa Maombi na Dua ya Kumwombea Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Amani katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Hanje amesema ana dhamira ya dhati ya kuwatumikia wananchi wa Singida Mashariki.

Ameeleza kuwa nia yake ya kugombea inatokana na hamu ya kuwasaidia wananchi, huku akisisitiza kuwa ubunge wake hautakuwa kwa ajili ya kujitajirisha.

"Nafikiri mtapata Mbunge ambaye kwa mara ya kwanza mtafurahia kuwa naye, kwa sababu sijapanga kutajirika kupitia Ubunge. Nitahakikisha ninagawana nanyi kadri inavyofaa," amesema Hanje.

Hawa ndugu wamechanganyikiwa. Hawaelewi hata wafanye nini. Hapo anatangaza atawania Ubunge, lkni hasemi atawania ubunge kupitia chama gani. Kinachoonekana ni Bendera za Tanzania zenye picha ya Rais. Hiyo nayo itakua bendera mpya mjini. Dada zetu hao wamekua kama mpira uliotumiwa , baada ya tendo la ngono, ukatupwa jalalani.

Hanje, ukipita hapa, chukua ushauri huu, achana na biashara ya ubunge kwa sasa, toka mafichoni, kivue kivuli chako uweke wazi mapenzi yako ya chama. Kuwa mwana CCM sio dhambi lakini kuwa ndumilakuwili ni kosa la kimantiki.
 
Mkuu siku hizi naona kichwa chako kimepoteza focus kabisa. Chuki iliyonayo kwa Lissu inakufanya hata uone ni bora Samia ateue wabunge wote wa Tanzania kuliko Lissu kupata tena ubunge. Hili jambo huwa linanishangaza sana. Watu wengi walio upinzani wanapotofautiana na wenzao wanakuwa wabaya kuliko hata CCM.
Kuna watu wengi timu Mbowe bado wamenuna sana mpaka sasa!
 
Back
Top Bottom