Mbunge wa Hai ndugu Saashisha Mafuwe amekuwa source ya mgogoro kati ya muwekezaji wa makoa farm na wananchi wa kijiji cha uduru ambao ndiyo wamiliki wa shamba hilo. Muwekezaji huyo mjerumani aitwaye Elizabeth ana mkataba wa uwekezaji unaofika ukomo mwaka 2039.
Mapema mwezi huu mbunge SAASHISHA alikodi genge la wahuni pamoja na baadhi ya wanamgambo wa Mrusi aitwaye Alex (alteza) ambaye Saashisha anampigia chapuo apewe shamba hilo la MAKOA, walimvamia muwekezaji huyo ili kumtisha akimbie na kuliacha shamba mwishowe waliishia kuburuzwa mahakamani mbunge akiwa ni mshitakiwa namba moja.
Jana alhamis Mbunge alikuwa na kikao nyumbani kwa mwenyekiti mstaafu wa CCM wilaya ya Hai Ndugu AMINI ATHUMAN URONU ambapo walikusanywa makada wa CCM. ajenda ya kikao hicho ni kuwatumia wananchi wa kijiji cha nshara hususani kitongoji cha nnyama ambacho kina makada wengi wa CCM kufanya jaribio lingine la kumvamia muwekezaji huyo.
Na katika kikao hicho mbunge aliweka wazi kuwa lengo ni kuhakikisha kuwa muwekezaji Alex (alteza) aliyewekeza kwenye hotel ya Aishi inayomilikiwa na Mbowe anaondoka kwa Mbowe na kuhamia kwenye shamba hilo la makoa farm. Ili kumpunguza nguvu Mbowe.
Maswali ya kujiuliza
1. Kama mbunge anaona muwekezaji Eliza kuna masharti ya mkataba ameyakiuka, ni kwa nini asiwashauri wananchi kutumia njia sahihi ili kuvunja huo mkataba badala yake anatumia njia haramu?
2. Ni nini kilicho nyuma ya pazia kwenye mgogoro huu?
3. Ni kwa nini jana afanye kikao na wananchi wa kijiji cha nshara ambao siyo sehemu ya mgogoro huo au siyo wamiliki wa shamba hilo ili tuu kuwaingiza kwenye mgogoro usiowahusu?
Kwa kumalizia tunaomba TAKUKURU waingilie na kuchunguza mgogoro huu kabla damu za wana Hai hazijamwagika kwa sababu ya maslahi binafsi ya mbunge Mafuwe.