TANZIA Mbunge wa Jimbo la Konde Zanzibar, Khatib Haji afariki Dunia

TANZIA Mbunge wa Jimbo la Konde Zanzibar, Khatib Haji afariki Dunia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Mbunge wa Jimbo la Konde Ndugu, Khatib Haji wa Chama cha ACT Wazalendo, amefariki Dunia. Umauti umemfika katika Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili akipatiwa matibabu Alfajiri ya leo.

Khatibu aliwahi kuwa Mbunge wa Konde kupitia Chama cha Wananchi CUF mwaka 2010 hadi 2020. Alishawahi kushika nafasi ya Waziri wa Kilimo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mwaka 1984 hadi 1987

Katika Bunge hili la 12, Khatib amekuwa Mbunge wa tatu kufariki tangu Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020. January 21 2021 Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mkoa wa Manyara, Martha Umbulla alifariki dunia na Feb 12, 2021 Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, Mkoa wa Kigoma Atashasta Nditiye alifariki Dunia baada ya kupata ajali ya gari.

Mbunge.jpg

Mbunge wa Jimbo la Konde Ndugu, Khatib Haji

691E91E1-850C-4971-8F41-4A51E694A487.jpeg
 
Pole kwa familia yake na wa-Zanzibar kwa ujumla.

Zitto amekuwa mnafki na amekuwa kama tissue ya CCM, ni ngumu kumpa pole Zitto, labda watu wengine. Ndiye anachangia kuua upinzani Tanzania na kuendelea kuongozwa kimabavu.
 
Pole kwa familia yake na wa-Zanzibar kwa ujumla.

Zitto amekuwa mnafki na amekuwa kama tissue ya CCM, ni ngumu kumpa pole zitto, labda watu wengine. Ndiye anachangia kuua upinzani Tanzania na kuendelea kuongozwa kimabavu.
Uko sahihi. Zito ni shetani wa upinzani, tena afadhali ya CCM kuliko Zito
 
Season 3 imeshaingia ndugu zangu tukae mkao wa kula sasa
 
Back
Top Bottom