Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,281
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.

======

UPDATES; 00:15HRS
Screenshot from 2018-07-31 00-22-02.png

Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi Rais Magufuli. Amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole.

Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi," Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.

Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015
 
Last edited by a moderator:
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
 
Last edited:
Tatizo sababu wanazozitoa kwa kuhama kwao huwa hazina mashiko yoyote yale na badala yake zinawavua nguo na kuonesha ni kwa vipi hawawezi kutumia baraka waliyopewa na mungu za kuwa binadamu badala ya Ng'ombe!!
Kule atapewa ukuu wa mkoa. Anaweza hata awe waziri mkuu
 
Back
Top Bottom