Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.
Wakolomije watambue CDM ilikuwa na Wabunge Wanne tu kina Zitto na Slaa etc enzi hizo na ikavuma,kwa sasa wapo wengi,wameondoka hao wa3 bado wapo Majembe ya kutosha yasiyoyumba,ni kipindi cha mpito tu hiki,wachumia tumbo wanajichuja wenyewe vipande 250m vya fedha unauza utu.
 
Siasa bana..
Mtu anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingne wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingne wanaonekana wasaliti vilevile

Mkuu kama una namba yake, mshauri amsihi Lowassa warudi wote ccm. Wameifubaza cdm.
 
Waende tu bwana kwani shida iko wapi? Hata Mbowe mwenyewe akitaka kuhamia huko aende tu, wala mimi asiniage kabisaaa,, tutabaki tunaojitambua! Mimi atakayeniliza akihamia CCM ni Lissu tu zingine hizi ni takataka tu (Kwa sauti ya Jacob)
 
Last edited:
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.
Aende tuuu naye huyo sioni la maana maana alihamia huko kwa mzimuuuu
Watu walio chama chetuu waturudii tuuuu chamani kwetu
 
Write your reply...Duuh, is this a price of democracy?
 
Sidhani kama kuna usahihi maana yule mlezi wake ni Lowassa. Hawezi kuhama hivi hivi maana Lowassa ataonekana ameshindwa kisiasa.
 
Sasa wana shambulia ngome ya lowasa huku wana endelea na mashambulizi kwenye ngome ya mbowe pale Hai
Kuna haja ya wanazuoni wa kimataifa si hawa wa bongo kuja kuitafiti aina mpya ya siasa tunayoiendesha hapa tz ni kwa faida ya vizazi vijavyo..lakini tanzania ni ya pili kwa vivutio vya utalii duniani si mbaya kuongeza utalii wa siasa pia
 
Back
Top Bottom