Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Bora iwekwe sheria mtu ahame na cheo mana hakuna aliye hama akakosa ushindi hii itasaidia kuokoa pesa za watanzania masikini .
 
Ndio madhara ya rubani kubadilisha gia angani. Tangu lini uliona gia inabadilishwa angani? Wacha lidege liporomoke tu.
 
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
Say no more...mkuu
 
Kwahiyo waitara ndio alikuwa anakatwa peke yake? Waitara alikuwa kirusi since wayback(M2) kabla hata hajakuwa Mbunge.
Basi kamuulize Lowassa au Sumayi kama humwaamini Waitara au wale wabunge wengine waliohama hicho chama cha saccos.
 
Basi kamuulize Lowassa au Sumayi kama humwaamini Waitara au wale wabunge wengine waliohama hicho chama cha saccos.
Wabunge wanaohama kwenda CCM ni wachumia tumbo kwa sababu moja tu,wanaenda kugombea tena nafasi ile aliyoiacha,nitawaamini endapo wakiondoka upinzani na kutogombea tena,muangalie nyalando kaacha katulia kimya anafanya mambo yake.
 
Nchi zote zilizopiga hatua kubwa katika maendeleo ya kiuchumi kisiasa wana vyama Vikuu angalau viwili vya siasa. USA, EUROZONE JAPAN, INDIA NK. China pamoja nakuwa na Chama kimoja walijiwekea utaratibu wa kuingia timu mpya ya uongozi kila baada ya miaka 10, ingawa utaratibu huu wsmeuondoa kwa Rais wa nchi!
 
Viongozi wa upinzani hasa Chadema wanajisahau kuwa wao sio sawa na mwenyekiti wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM na wale wa vyama vya upinzani ni kama mbingu na ardhi.
Mwenyekiti wa CCM akiwalazimisha wanachama wake kupigia kura bajeti analenga kutimiza malengo ya serikali yake.
Lakini wale wapinzani kila mwaka wanalazimishwa kupinga bajeti bila kutuambia wanataka ipitishwe ipi ?
Yani wanataka nchi isiwe na bajeti au wanataka nini na uchache wao?

Mwenyekiti wa Chadema akimbana Mwanachama wake wakati mwingine mtu anaona isiwe tabu naweka maisha yangu rehani halafu bado nabughudhiwa na kutishwa tishwa na mtu asiye na teuzi zaidi ya viti maalum.
Mwenyekiti wa CCM akimtishia mtu ujue kweli mtu anapata tabu sana mana fursa zote za nchi hii zipo mikoni mwake. Sasa mwenyekiti wa Chadama ana nini cha kumtishia mtu mpaka mtu aufyate?

Mbowe ajaribu sasa kusikiliza watu wa maeneo mengine nje ya wale wa waliomzunguka ambao wanaangalia maslahi yao kwanza.
Vinginevyo chama kitapukutika kabisa.
Watanzania hawana uelewa huo wanaoufikiria wapinzani.
Wengi wanaamini kuwa juhudi za Mh. Rais zinavunja nguvu ya vyama vya upinzani. Watapinzani wamejisaha kabisa.
Ngoja wabunge wao waishe ili wajipange upya.
 
Mjinga tu yule. Amekanusha nadhani hajakabidhiwa hela bado.
 
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
Kosa ni la wapiga kura kwani cha mlevi huliwa na mgema.
 
Wakuu kwa wale walio Macho muda huu bila kubanwa na shughuli za kifamilia.. Hebu jongea kwenye account ya Mhe pole pole ya tweeter na face upate live feeds... Ameanza muda huu..
Pata updates za utekelezaji wa Miradi na shughuli za serikali.
Na ilani ya chama pia.
Screenshot_20180730-235935.jpg
 
Back
Top Bottom