Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Wabunge wanaohama kwenda CCM ni wachumia tumbo kwa sababu moja tu,wanaenda kugombea tena nafasi ile aliyoiacha,nitawaamini endapo wakiondoka upinzani na kutogombea tena,muangalie nyalando kaacha katulia kimya anafanya mambo yake.
Hapa duniani hakuna binadamu ambaye si mchumia tumbo. Hata mimi na wewe sote ni wachumia tumbo. Ila binadamu wengine wamezidi mno!. Yaani ruzuku yote ya chama kila mwezi inaenda kwenye tumbo moja kulipia madeni hewa yasiyoisha. It is just too much 'uchumia tumbo'!
 
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi @ccm_tanzania muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi za Mh.Rais Dkt @MagufuliJP. Darmpya on Twitter
IMG_20180731_001610.jpg
 
Shida sio kuhama chama ,bali shida ni mabilioni ya pesa ya kodi za wananchi wanyonge yanayotumika kurudia uchaguzi.
 
Viongozi wa upinzani hasa Chadema wanajisahau kuwa wao sio sawa na mwenyekiti wa CCM.
Mwenyekiti wa CCM na wale wa vyama vya upinzani ni kama mbingu na ardhi.
Mwenyekiti wa CCM akiwalazimisha wanachama wake kupigia kura bajeti analenga kutimiza malengo ya serikali yake.
Lakini wale wapinzani kila mwaka wanalazimishwa kupinga bajeti bila kutuambia wanataka ipitishwe ipi ?
Yani wanataka nchi isiwe na bajeti au wanataka nini na uchache wao?

Mwenyekiti wa Chadema akimbana Mwanachama wake wakati mwingine mtu anaona isiwe tabu naweka maisha yangu rehani halafu bado nabughudhiwa na kutishwa tishwa na mtu asiye na teuzi zaidi ya viti maalum.
Mwenyekiti wa CCM akimtishia mtu ujue kweli mtu anapata tabu sana mana fursa zote za nchi hii zipo mikoni mwake. Sasa mwenyekiti wa Chadama ana nini cha kumtishia mtu mpaka mtu aufyate?

Mbowe ajaribu sasa kusikiliza watu wa maeneo mengine nje ya wale wa waliomzunguka ambao wanaangalia maslahi yao kwanza.
Vinginevyo chama kitapukutika kabisa.
Watanzania hawana uelewa huo wanaoufikiria wapinzani.
Wengi wanaamini kuwa juhudi za Mh. Rais zinavunja nguvu ya vyama vya upinzani. Watapinzani wamejisaha kabisa.
Ngoja wabunge wao waishe ili wajipange upya.


Yaani wewe mpaka leo hii hujui kwamba bajeti mbadala ya upinzani iko kikatiba na kisheria?
Unadhani wanajitungia tu?
 
Back
Top Bottom