Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Elections 2015 Mbunge wa Jimbo la Monduli, Julius Kalanga (CHADEMA), ajiuzulu na kuhamia CCM

Tumeshawaambia chadema siku nyingi, hizo siasa za kupinga kila kitu siyo za kistaarabu na haziwezi kuwasaidia chochote. Matokeo yake ndo haya wabunge wanajiondoa ili kuepuka kuonekana ni wasaliti kwa chama kwa kuunga mkono jitihada zinazofanywa na serikali ili kuleta mabadiliko nchini. Usingizi wa siasa za chuki za #lissumsaliti zitawamaliza.
Kuunga mkono nini? na kwann wasiende vyama vingine kama Tlp na CCj ili tujue hawajanunuliwa huuu ni ufisadi wa kijinga at excited state tumechoka hela hakuna alaf watu wanatumia hovyo
 
hameni tena hameni na rafiki zenu mpaka majirani
jioni ikifika kila kuku hurudi kwenye makazi aliyoyazoea sasa naona muda ndo huu
mwisho Wa cku kila mtu atarudi ktk nafasi aliyoizoea
 
Siasa bana..
Mbunge / anahama chama kwa madai kwamba wabunge wa upinzani wanalazimishwa kupinga bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti alafu unahamia chama ambacho wabunge wanalazimishwa kupitisha bajeti na wakifanya vingine wanaonekana wasaliti vilevile
fact sana mkuu. Mimi nadhani tuna gap kubwa sana katika kuwatengeneza viongozi wetu kama taifa
 
Chadema wanatakiwa kufanya marekebisho sio kudanganya watu kua kila anaehama kanunuliwa
very great idea. Mimi nadhani hiyo ndo fact number moja kwa CHADEMA kwa sasa.
Restructuring ya chama ni muhimu kwa sasa na sio kukimbia na media na kusema watu wamenunuliwa.
Hivi wakiondoka wabunge 20 kwa awamu hii moja tu watakuwa wamenunuliwa wote?

Just thinking loud
 
Wewe ni mtu wa ajabu sana. Hivi hujui kuchafua uchaguzi halali ni kosa?? Kwa sheria hiyo hiyo ya kuuchafua uchaguzi huru na wa haki.
Hiyo fedha wangelikuwa wanatozwa ili kuufanya uchaguzi mardio nadhani wangeshika adabu yao
Nenda mahakamani usiishi kwa majungu
 
Kwa mwendo huu, na viongozi wa namna hii, nasema Ulaya, Amerika na Asia...wakisema wasimame walipofikia kimaendeleo watusubiri sisi tu hata tukipewa miaka 1000+ hatutawafikia ng'o
 
Naona tunarud kwenye Zle kula za ndiyo au hapana..NAHISI NDIYO WAMESHINDA
 
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya Mkoa wa Arusha zinasema Mbunge wa Jimbo la Monduli Juliasi Kalanga kuhamia CCM kesho majira ya saa nne asubuhi.

======

UPDATES; 00:15HRS
View attachment 823188
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Monduli kwa Tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) , Mhe. Julius Kalanga amejiuzulu na kujiunga na Chama cha Mapinduzi CCM muda huu kwa kile alichoeleza kuwa ni kuunga mkono juhudi Rais Magufuli. Amepokelewa na katibu mwenezi wa CCM ndugu Humphrey Polepole.

Siasa za uhasama, malumbano na chuki zimeniondoa CHADEMA. Nimeamua kuiunga mkono serikali ya awamu ya tano kwa maslahi ya taifa... Kwa sababu huwezi kufanya hivyo ukiwa upande wa pili, lazima utaonekana msaliti tu... Wana Monduli naombeni mnielewe, nitakuja kuzungunza nanyi," Julius Kalanga Laizer, aliyekuwa Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CHADEMA.

Julius Kalanga aliwahi kuwa diwani kupitia CCM, kabla ya kuhamia Chadema 2015
Nenda na mamilioni uliyopewa, wananchi bado wao wanataka mabadiliko na katiba mpya.
 
Unapijiona huenei popote hata pale ulipo dawa yake ondoka kimyakimya achana na visingizio,kumbuka kuna maisha baada ya leo(kesho ipo na ina mambo yake pia)
 
Hahahahahaha jiwe na polepole mnaweza chezea pesa ya wanamchi kulazimishwa kipendwa wakati huohuo mnazuia uchaguzi usiwe huru
Assumption! Hapo ndo tujiulize ubora wa akili ya watu walioko huko Bungeni. Je, wanajifahamu? HAta kama kuna pesa inatumika, ni lazima ukubali kila kitendo kwa sababu ya pesa? Hakuna sababu ya kuwalaani changudoa.
 
Back
Top Bottom