Mbunge wa Jimbo la Ole, Pemba asema nyama iliyoteketezwa ilikaa muda mrefu baharini ikaharibika

Mbunge wa Jimbo la Ole, Pemba asema nyama iliyoteketezwa ilikaa muda mrefu baharini ikaharibika

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Mei 29, 2026 Mdau aliandika “Pemba: Nyama ya msaada iliyotolewa na Wabunge imebainika haifai, kuna watu wameingia nayo mtaani, Mamlaka zipo kimya”

Hoja ya awali ~
Pemba: Nyama ya msaada iliyotolewa na Wabunge imebainika haifai, kuna watu wameingia nayo mtaani, Mamlaka zipo kimya

Mbunge wa Jimbo la Ole, Mhandisi Said Salim, ametoa ufafanuzi kuhusu tukio hilo na kueleza kuwa nyama iliharibika kutokana na kukaa muda mrefu baharini na ilipobainika haifai iliteketezwa yote.
photo_2026-05-31_08-07-02.jpg
photo_2026-05-31_08-07-00.jpg
Safari ya nyama hiyo
Mhandisi Said Salim amebainisha kuwa mzigo huo wa nyama ulisafirishwa halali ukitokea mkoani Tanga kuelekea Pemba ukiwa na nyaraka zote zinazohitajika, ikiwemo Leseni na vibali vyote vya usafirishaji, muhuri rasmi wa daktari unaothibitisha ubora wa nyama.

Hata hivyo, tofauti na safari za kawaida za mashua zinazochukua kati ya saa mbili na nusu hadi saa tatu, safari hiyo ilikumbana na changamoto kubwa ya hali mbaya ya hewa na bahari kuchafuka.

Anasema "Kutokana na bahari kuwa chafu, mashua iliyobeba mzigo huo ilitumia muda mrefu sana baharini. Ilitoka Tanga saa 9:00 alasiri na kufika Pemba saa 3:00 asubuhi ya siku iliyofuata."
photo_2026-05-31_08-06-58.jpg
photo_2026-05-31_08-05-38.jpg
Ingawa mzigo huo ulikuwa umewekewa kiasi kikubwa cha barafu tani 1.5 (mifuko 300) kwa ajili ya uhifadhi, muda mrefu uliopotea baharini ulisababisha barafu hizo kuyeyuka na nyama kuanza kuonyesha dalili za kuharibika ilipowasili bandarini.

Udhibiti na Uteketezwaji wa Haraka

Mhandisi Said Salum amesema ulinzi ulikuwa mkali na hakuna mtu aliyechukua nyama hiyo na kuondoka nayo kwa kuwa hatua za dharura zilichukuliwa haraka mara baada ya mzigo huo kuwasili.

Anasema uliwasili Saa 3:00 Asubuhi na baada ya Wakala wa Chakula, Dawa na Vipodozi Zanzibar (ZFDA) kubaini kuwa hauko katika hali nzuri, mchakato ulifanyika na Saa 4:00 Asubuhi yaani ndani ya saa moja tu, mzigo wote ulikuwa umeshafikishwa kwenye eneo maalum la uteketezaji.

"Mchakato huo mzima ulifanyika chini ya usimamizi thabiti wa mamlaka za kiserikali na hakuna hata kipande kimoja cha nyama kilichoruhusiwa kutoka nje ya eneo hilo au kuingia sokoni," anasema Injinia.

Changamoto za Usafiri wa Baharini kwa Nyakati za Sikukuu
Mbunge huyo aligusia kuwa ajali na changamoto za kibahari zimekuwa zikitokea mara kwa mara, hasa nyakati za kuelekea sikukuu kutokana na mabadiliko ya ghafla ya hali ya hewa. Alitolea mfano wa hivi karibuni ambapo chombo kilichobeba ng'ombe kuelekea Pemba kilipinduka kutokana na dhoruba, na kusababisha wanyama wote kufa maji, huku manahodha wachache pekee wakiokolewa.

Hali hii inaonyesha kuwa changamoto iliyotokea kwenye mzigo wa nyama ilikuwa ni ya kimaumbile na dharura ya usafiri wa baharini, na si uzembe wa mamlaka au wafanyabiashara.
 
Mngekula tu hivyo hivyo ili mharishe hadi mkome na huo uroho wenu.
 
Back
Top Bottom