PreGE2025 Mbunge wa Jimbo la Pangawe Wananchi wako wanadai umewatupa

PreGE2025 Mbunge wa Jimbo la Pangawe Wananchi wako wanadai umewatupa

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
706
Reaction score
1,716
Wakazi wa Tawi la Mnarani, Jimbo la Pangawe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Wilaya ya Dimani, Unguja ni kama hawana tawi licha ya kwamba lipo na Wananchi wanalijua.

Nina mzee wangu ambaye yupo hapo analalamika kuwa jengo ambalo wamepanga kodi iliisha tangu Desemba 2024, lakini kinachowasikitisha zaidi ni kuwa Mbunge wao hajawahi kuwasaidia hata mara moja.

Anadai kwamba anayewawezesha ni Mwakilishi ambaye yupo katika Baraza la Wawakilishi, Mwakili wa Jimbo la Pangawe - Ali Suleiman Mrembo.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Wananchi na hasa wale wa Kada wanajiuliza mbona mbunge wao Huyu mbunge wao wanajiuliza anategemea nini au ndio hataki tena kugombea, mbona anawapotezea sana?

Maana kwa jinsi anavyowapotezea ni kama vile hataki tena kura zao, wanamsisitiza afanye jambo kwa kuwa yupo nje ya muda.
WhatsApp Image 2025-03-18 at 16.24.30_fb5595cd.jpg
 
Back
Top Bottom