Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Mmawia

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2013
Posts
122,494
Reaction score
96,074


Mbunge wa Kahama Mjini kupitia CCM Jumanne Kishimba, ameiomba Serikali ifungue chuo cha wizi kwa kuwa matukio ya wizi katika sekta za umma na Halmashauri nyingi umeshamiri kwa kiasi kikubwa na kwamba chuo hicho kitasaidia wale watu wanaoenda kuchunguza wezi, kuzijua mbinu zao na kuwabaini.

Hayo ameyabainisha leo Mei 28, 2020, Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa 19, kikao cha 39, wakati wa uchangiaji wa hoja ya Kamati ya Kudumu ya Huduma za Serikali za Mitaa, na kueleza kuwa ni vyema chuo hicho kikawekwa japo kwa kutumia jina lingine ili kukomesha suala hilo.

"CAG na Waziri wa Fedha yuko hapa hawa vijana wanaoajiriwa lazima wanatoka shule inayofundisha maadili mema na uaminifu, sasa wanaenda kupambana na wizi wengine wamesoma Seminari, kwanini serikali haifikirii sasa kuanzisha chuo cha wizi, kwa maana mtu anapochaguliwa kwa sifa ya uaminifu kwenda kupambana na wezi anaenda kupambana nao namna gani? afadhali apite kwenye chuo hicho kwa miezi mitatu ili ajue akili ya wizi, hawa vijana wetu tutawamalizia magerezani na hali ya wizi ni mbaya sana" amesema Mbunge Kishimba.

Credit: EATV

Mwaka jana, Kishimba alitaka kilimo cha bangi kihalalishwe nchini Tanzania Mbunge Jumanne Kishimba (CCM) ataka kilimo cha bangi kuhalalishwa nchini Tanzania

Maoni Yangu
Kumbukeni huyo mbunge alishawahi kuomba Serikali iruhusu bangi itumike kihalali.

Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.

Kama taifa bado tuna safari ndefu.
 
Mbunge wa kahama Jmanne Kishimba ameishauri serikali kuanzisha chuo cha wizi ili kila mtumishi ajue kuiba kisomi.

Kumbukeni huyo mbunge alisha wahi kuomba serikali iruhusu bangi itumike kihalali.

Daaaa hao ndiyo wabunge wetu ambao ni watunga sheria na wapitisha miswaada na mikataba mbali mbali.

Kama taifa bado tuna safari ndefu.

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa huyu Mbunge aliwahi kuomba sheria ya wazazi kuwashitaki watoto wasipowatumia fedha
 
Huyu mbunge toka nimeanza kumjua hajawahi ongea point kamwe. Anyway ni haki yake kutoa maoni wako wabunge wako bungeni wanakula posho na kodi zetu bure tu
 
Ana hoja ya Msingi lakini kashindwa tu kui frame vizuri

Utawezaje kupambana na tatizo ambalo hulijui?

Mf. Kwenye Course za upelelezi siku zote unafundishwa namna mbali mbali na mbinu za kufanya uhalifu na kuficha uhalifu halafu unafundishwa technique za kutambua
 
Back
Top Bottom