Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Kama kumbukumbu zangu zipo sawa huyu Mbunge aliwahi kuomba sheria ya wazazi kuwashitaki watoto wasipowatumia fedha
Yes ni yeye, na mwenyekiti wa bunge (A. Chenge) alimtania 'profesa Kishimba' wakati akihitimisha mchango ule.
 
Naona jinsi alivyowasilisha hoja ndio tatizo,lkn kuna point ndani yake

Yaani kuwe na chuo ambacho wajifunze mbinu/njia mbalimbali sina zotumika kuiba kama alivyotolea mfano wa jeshi la polisi kuijua silaha nao wanatakiwa wapate ujuzi huo

Hii yote ni katika kudhibiti wizi wa umma
 
Hivi Kishimba huyu ni yule wa Imaraseko super Market?
Yes ni yeye, na mwenyekiti wa bunge (A. Chenge) alimtania 'profesa Kishimba' wakati akihitimisha mchango ule.
 
Ana hoja ya Msingi lakin kashindwa tu kui frame vizuri

Utawezaje kupambana na tatizo ambalo hulijui?

Mf. Kwenye Course za upelelezi siku zote unafundishwa namna mbali mbali na mbinu za kufanya uhalifu na kuficha uhalifu halaf unafundishwa technique za kutambua
Sijamsikia alivyo wasilisha, ila uko sahihi. Kwenye Security tunasema 'It takes a thief to catch a thief' ndio maana tunajifunza 'ethical crimes'.
 
Jamaa alikuwa dereva wa lori Scania la Mizigo la SHIRECU , halafu akaiba nadhani ngano aliyokuwa akisafirisha kutoka Dar kwenda Shinyanga kwa kuangusha gari Singinda na kuuza ngano yote katika utaratibu ambao haukuacha trace yoyote ya ushahidi. Baada ya hapo akaacha udereva na kuanza biashara ya kusaga nafaka na usafirishaji mizigo;

Baadaye akawa tajiri wa kutupwa na kuanza kumiki mali zote zilozokuwa za KADECO wakati wa miaka ya themanini. Kuna mantiki ya step tatu katika ushauri huu: iba-usishikwe-rudisiha kwa jamii. Jamaa ameisadia sana Kahama kuliko enzi hizo za KADECO.
 
Kama CCM kitaendelea kuwa madarakani nchi hii haiwezi kuendelea kamwe, uwezo wao kiutendaji, kiutekelezaji, kimipango ni sifuri. yaani wamekosa kabisa vision & mission ya kuiendeleza nchi hii.
 
Jamaa alikuwa dereva wa lori Scania la Mizigo la SHIRECU , halafu akaiba nadhani ngano aliyokuwa akisafirisha kutoka Dar kwenda Shinyanga kwa kuangusha gari Singinda na kuuza ngano yote katika utaratibu ambao haukuacha trace yoyote ya ushahidi. Baada ya hapo akaacha udereva na kuanza biashara ya kusaga nafaka na usafirishaji mizigo; baadaye akawa tajiri wa kutupwa na kuanza kumiki mali zote zilozokuwa za KADECO wakati wa miaka ya themanini. Kuna mantiki ya step tatu katika ushauri huu: iba-usishikwe-rudisiha kwa jamii. Jamaa ameisadia sana Kahama kuliko enzi hizo za KADECO.
Huyu si ndiyo alikuwa na meli yake ya mizigo ikaungua ziwani?
 
Watu kama hawa kamwe hawawezi kukosekana ndani ya CCM maana ndiyo mtaji wao mkubwa.

Angalia mikataba tata yoote ya madini ambayo leo hii Jiwe anaitolea macho ilipitishwa na wabunge hao hao.

Zitto na Mnyika na Lissu alipinga sana na kushauri namna ya mikataba inatakiwa iwe lkn walionekana ni wasaliti.
kama CCM kitaendelea kuwa madarakani nchi hii haiwezi kuendelea kamwe, uwezo wao kiutendaji, kiutekelezaji, kimipango ni sifuri. yaani wamekosa kabisa vision & mission ya kuiendeleza nchi hii.
 
Huyu si ndiyo alikuwa na meli yake ya mizigo ikaungua ziwani?
Sijui; kumbukumbu niliyotoa ni ya zaidi ya miaka 30 iliyopita, inaweza kuwa sahihi au sivyo kwa vile kama nilivyosema haikuacha trace zozote za ushahidi physical bali ilikuwa ni circumstantial tu ambayo ikawa ngumu kufuatilia kutokana na matukio mengine yaliyohusu uongozi wa Shirecu wakati huo. Usimhukumu kwa taarifa hii
 
1. Huyo mtu ni darasa la saba ila kaongea kitu ambacho hata maprofesa hawawezi kumuelewa na ndicho kinachoonekana hapa

2. Watu waliopitia vyuo vya kuwaandaa wachungaji na mapadre watakubaliana na mimi kuna somo huwa wanafundishwa kuwa hakuna Mungu na wanasoma phylosopher wengi wanaokataa uwepo wa Mungu ila miaka ijayo ndio wanakuja kusoma kuwa Mungu yupo.

3. Anachomaanisha kuwa huwezi kugundua mwizi kama hujui mbinu anazotumia hivyo inatakiwa wajifunze hizo mbinu na namna ya kukabiliana nazo zisitokee katika idara yake.

4. Kumbuka kuwa unapochaguliwa kuwa kiongozi unakuwa ndio mkuu wa idara zote zenye taaluma tofauti kabisa na ulichokisomea na likiharibika jambo huna utetezi kuwa hukusomea.

5. Asilimia kubwa ya viongozi wanaotumbuliwa unakuta kosa limefanywa na mtaalamu katika idara fulani au kamuingiza mkenge bosi wake hivyo ni muhimu viongozi kabla hujawa overol incharge wa idara zote ikiwemo uhasibu, manunuzi na store ujue abc ya mbinu wanazotumia kuiba ili uweze kupambana nao
 
Back
Top Bottom