Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Mbunge wa Kahama Mjini(CCM), Jumanne Kishimba ashauri Serikali kuanzisha chuo cha wizi

Nimekuelewa mkuu
Sijui; kumbukumbu niliyotoa ni ya zaidi ya miaka 30 iliyopita, inaweza kuwa sahihi au sivyo kwa vile kama nilivyosema haikuacha trace zozote za ushahidi physical bali ilikuwa ni circumstantial tu ambayo ikawa ngumu kufuatilia kutokana na matukio mengine yaliyohusu uongozi wa Shirecu wakati huo. Usimhukumu kwa taarifa hii
 
Inasikitisha Sana Huyu mbunge anasema vijna ni wezi, vijana wakipewa ajira wanaiba.
 
Kishimba hajakosea, ila ni mtu ambaye uwezo wa kuweka mawazo yake kisomi una matatizo, kwa wanaoelewa ametoa mchango mkubwa sana.

Anacho maanisha serikali iwekee mkazo kwenye Theft forensic audit (Forensic Audit - means accounts examination, enquiry, exploration, analysis, appraisal, sifting, fact finding.

Kwa nilivyo muelewa, hasa nikifuata Collate method- yaani mtu anatamka anacho fikiria ,kwa mpangilio anao weza yeye halafu wataalamu wanaweka katika mpangilio wa kisomi.

Lakini kupambana na wizi it is more of ethos. Jamii ilikwisha hama katika uadilifu. Siku hizi mwizi anaheshimiwa.
 
Jamaa alikuwa dereva wa lori Scania la Mizigo la SHIRECU , halafu akaiba nadhani ngano aliyokuwa akisafirisha kutoka Dar kwenda Shinyanga kwa kuangusha gari Singinda na kuuza ngano yote katika utaratibu ambao haukuacha trace yoyote ya ushahidi. Baada ya hapo akaacha udereva na kuanza biashara ya kusaga nafaka na usafirishaji mizigo; baadaye akawa tajiri wa kutupwa na kuanza kumiki mali zote zilozokuwa za KADECO wakati wa miaka ya themanini. Kuna mantiki ya step tatu katika ushauri huu: iba-usishikwe-rudisiha kwa jamii. Jamaa ameisadia sana Kahama kuliko enzi hizo za KADECO.
Usisahau alivyoua watu na meli yake ya kaongo iliyozama kwa kupakia mizigo kuzidi uwezo wake. Serikali ilimlinda kwa nguvu zote alijificha Malawi kwa miezi sita aliporudi akagombea ubunge.
 
Sawa sawa nalikumbuka sana hilo tukio nafikiri kati ya mizigo iliyo kuwepo ni cement kibao
Usisahau alivyoua watu na meli yake ya kaongo iliyozama kwa kupakia mizigo kuzidi uwezo wake.Serkali ilimlinda kwa nguvu zote alijificha Malawi kwa miezi sita aliporudi akagombea ubunge.
 
Nafikiri ni mawazo yake, jambo la msingi ni kutoa maoni mbadala wa haya ili kwapamoja yalinganishwe yepi bora zaidi.!🤓🤓
 
1. Huyo mtu ni darasa la saba ila kaongea kitu ambacho hata maprofesa hawawezi kumuelewa na ndicho kinachoonekana hapa

2. Watu waliopitia vyuo vya kuwaandaa wachungaji na mapadre watakubaliana na mimi kuna somo huwa wanafundishwa kuwa hakuna Mungu na wanasoma phylosopher wengi wanaokataa uwepo wa Mungu ila miaka ijayo ndio wanakuja kusoma kuwa Mungu yupo...
Hiyo point yako ya namba mbili ni kiboko sana, nimeikubali
 
Huyu mheshimiwa ana uwezo wa kufikiri nje ya mfumo uliopo na kuwasilisha mawazo yake hata kama wote hamuyaamini...


"HE IS MY ROLE MODEL"

Nukuu: Kishimba

"Kama tumefanya business as usual na hakuna matokeo chanya kwa nini tusijaribu kufanya maamuzi kinyume na mazoea yetu..."

Tuna wajibu wa kufikiri na kutenda tofauti ili tupate matokeo tofauti...HASA VIJANA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona kaongea point, naona yupo innovative

Kama kwenye cyber crimes mfano Kwenye udukuzi ili uweze kumkamata mdukuzi lazima uwe umesomea udukuzi, Kwa kwanini mtu asijifunze mbinu za wizi ili awakamate wezi?!

Nadhani wengi hamkumwelewa ndo maana mnamshangaa.
 
Huyu mbunge toka nimeanza kumjua hajawahi ongea point kamwe. Anyway ni haki yake kutoa maoni wako wabunge wako bungeni wanakula posho na kodi zetu bure tu
mkuu hiki alichokiongea ni konki, sema hujamsoma fresh tu!
 
Binafsi nakubali mambo mengi anayochangia, namuunga mkono suala la bangi, namuunga mkono ktk hili pia. Ukitaka mwalimu wa chekechea au madarasa ya awali awe mzuri kiufundishaj ni lazma ugeuze akili yake awe km mtt ili aendane na wtt, huez kubaki na akili yako ya Masters ukafundishe huko.

Ili kumkamata mwizi ni lazma ukajifunze mbinu wanazotumia, tena ww ujifunze wizi haswaa na uwe mwizi zaidi yao ndipo utakapojua mbinu na namna ya kuwakamata vizuri. Ni sawa na yeyote anayesomea shahada ya ubobevu ktk fani yoyote! Kishimba yupo sahihi sana.
 
Back
Top Bottom