View attachment 2730559
Ni ajabu lakini ni kweli.
Huyu umwonaye hapo ☝️☝️juu ni mbunge wa Jimbo la Kahama Mjini maarufu kama
Prof. Ramadhani Kishimba...
Leo amekuwa miongoni mwa maelfu ya wananchi waliohudhuria mkutano wa mwisho siku ya leo wa Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa ndugu Tundu Lissu katika
OPERESHENI +255 KATIBA MPYA, OKOA BANDARI ZETU..
Mkutano huo ndo tu umemalizika muda si mrefu katika kata ya Isaka - Kahama ilipo bandari kavu (dry port ya Isaka iliyo chini ya TPA) ambayo nayo ni miongoni mwa walizopewa DP World..
Pamoja na uwepo wake pale, Tundu Lissu hakumkopesha hata kidogo kuhusu ushiriki wake wa kupitisha mkataba wa ugawaji wa bandari za Tanganyika Kwa waarabu wa Dubai kupitia kampuni yao ya DP World..
Video nzima ya hotuba hiyo itakujia si muda mrefu🙏