Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE WA KALIUA MHE. ALOYCE KWEZI AMPONGEZA RAIS SAMIA SULUHU HASSAN KWA MIAKA MIWILI MADARAKANI
Mbunge wa Jimbo la Kaliua, Tabora Mhe. ALOYCE KWEZI amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutimiza Miaka Miwili Madarakani huku akiainisha utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika Jimbo la Kaliua katika ya Oktoba 2020 hadi Disemba 2022.
Jimbo la Kaliua lina Tarafa Tatu (3) Kata 13 na Vijiji 55. Katika kipindi cha Miaka Miwili ya Rais Samia kukaa madarakani utekelezaji wa miradi ya kimaendeleo umefanyika ambapo zaidi ya Shilingi Bilioni 60.2 zimetolewa na Serikali Kuu.
✅ MIRADI YA UJENZI WA HOSPITALI YA WILAYA NA VITUO VYA AFYA
Shilingi Bilioni 3.0 zilitolewa kwa ajili ya Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Kaliua kujenga majengo 12, X-RAY mashine na Nyumba ya watumishi. Vilevile, Shilingi Milioni 648 zililetwa na Serikali Kuu kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha Afya Usinge.
Aidha, Shilingi Milioni 500 zilitolewa na Serikali kwa ajili ya Ujenzi wa Kituo cha Afya cha Igagala (Wodi, Theater, OPD na Maabara). Shilingi Milioni 130 Ujenzi kituo cha Afya cha Ukumbisiganga. Shilingi Milioni 479 Ujenzi wa Zahanati 7 zilizo maeneo ya Igombe, Usimba, Wachawaseme, Ugansa, Luganjo Mtoni, Usangi na Mkuyuni.
✅ MIRADI YA UJENZI MIUNDOMBINU YA ELIMU
Shilingi Bilioni 1.5 zilitolewa na Serikali Kuu kwa ajili ya Ujenzi wa Shule mpya tano (05) za Sekondari kama ifuatavyo: Usenye Sekondari (Milioni 475); Dr. John Pombe Magufuli Sekondari (Milioni 445); Jerry Mwaga Sekondari (Milioni 370); Usimba Sekondari (Milioni 86); Kasungu Sekondari (Milioni 120).
Aidha, Shilingi Bilioni 6.6 zilitolewa kwa ushirikiano wa Halmashauri, Wananchi, Serikali
Kuu, P4R, Mfuko wa Jimbo na TAWA kwa ajili ya ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 334 katika Shule za Msingi na Shule za Sekondari.
✅ MIUNDOMBINU YA BARABARA
1. Shilingi Bilioni 32 zilitolewa kupitia Wakala wa Barabara TANROAD kujenga Barabara ya lami kutoka Kazirambwa - Chagu yenye kilomita 36.
2. TARURA: Shilingi Bilioni 6 zilitolewa kujenga Barabara za lami na kuweka Taa barabarani Kaliua Mjini zenye kilomita 11.5 ambazo ni barabara za Ufukutwa, Kaliua na Ushokora.
3. Barabara za kimkakati zilizojengwa na zinazoendelea kujengwa ambazo zimegharimu jumla ya Shilingi Bilioni 2.3 ni kama zifuatazo;
A. Barabara ya Kazaroho: Nsimbo – Mpandamlowoka, Milioni 300
B. Barabara ya Usimba – Igombe, Milioni 300
C. Barabara ya Usinge – Mitomitano – Maboha, Milioni 200
D. Barabara ya Usinge - - Luganjo – Shera, Milioni 200
E. Kamsekwa – Kazaroho (German Milioni 400)
F. Wachawaseme – kombe, Milioni 160
G. Kaliua -Tuombe Mungu Mkuyuni, Milioni 250
H. Usimba – Magere, Milioni 20
I. Matengenezo: Sehemu Korofi na Karavati, Milioni 476
✅ UJENZI WA UKUMBI WA HALMASHAURI
Fedha kiasi cha Shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa ukumbi wa Halmashauri zilitolewa na Serikali ya Awamu ya Sita ambao kwa sasa Ukumbi umekamilika na unatumika kwa shughuli za Mikutano ya Halmashauri.
✅ MIRADI YA MAJI
Jumla ya Shilingi Bilioni 4 zilitolewa na Serikali ya Awamu ya Sita kwa ajili ya Ujenzi wa Miradi ya Maji katika Jimbo la Kaliua. Katika hili tunampongeza na Kumshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
A. Kijiji cha Isanjandugu; Milioni 67,269,421
B. Kijiji cha Bankoko; Milioni 70,584,124
C. Kijiji cha Usimba; Milioni 408
D. Kijiji cha Kazaroho, Imaramihayo na Nsimbo; Milioni 859,280,160
E. Kijiji cha Maboha na Miti Mitano; Milioni 438,806,250
F. Kijiji cha Wachawaseme, Mtakuja Magharibi & Mashaiki; Milioni 809,850,327
G. Kijiji cha Imarampaka; Milioni 92,089,992
H. Kijiji cha Ushokora; Milioni 213,281,095
I. Kijiji cha Mtakuja Magharibi; Milioni 99,999,869
J. Kijiji cha Mtakuja Mashariki-Kawawa; Milioni 70
K. Kijiji cha Usinga; Milioni 240
L. Utafiti wa maji na Uchimbaji wa Visima 11 katika Vijiji vya Usinge, Ugansa, Mpwaga,
Kamsekwa, Igwisi, Mpandamrowoka, Usimba, Kangeme, Lumbe, Mkuyuni na Limbulasiasa; Milioni 440
M. Upanuzi wa Mradi wa Maji Kaliua – Uwanja wa Ndege; Milioni 447
✅ MIRADI SEKTA ZA UCHUMI NA UTAWALA
A. Ujenzi wa Uzio wa Mnada wa Ng’ombe wa Ugansa
B. Ununuzi wa Pikipiki 13 kwa Watendaji wa Kata
C. Ujenzi wa vyumba vya Biashara 6 Stendi ya Mabasi
D. Ufungaji wa CCTV Camera eneo la Stendi kudhibiti udanganyifu
E. Ugawaji wa Miche 150,000 ya Michikichi kwa Wananchi
F. Uuzaji wa Mbegu za Alizeti; Tani 10 zimegawiwa
✅ MICHEZO JIMBO LA KALIUA
Shilingi Milioni 35. Seti za jezi za michezo zipatazo 220 na Mipira 220 kwa kila kijiji. Aidha, kila Kata ilipewa Shilingi 750,000/= kwa ajili ya mashindano ya Kata. Timu 32 zilipewa Seti ya jezi kila Timu na Mshindi wa kwanza alipatiwa Shilingi Milioni 3, Mshindi wa Pili Shilingi Millioni 2 na Mshindi Tatu Milion 1.
✅ MRADI WA MIKOPO 10%- WAMAMA, VIJANA & WALEMAVU
Shilingi Milioni 814,400,000 katika kipindi cha Miaka Miwili zilitolewa katika Jimbo la Kaliua ikiwa ni mgao wa 10% kutoka TAMISEMI ambapo jumla ya vikundi 118 vilinufaika.
✅ UJENZI WA MAHAKAMA YA WILAYA
Katika kipindi ncha miaka miwili tumefanikiwa kujenga Mahakama ya Wilaya ya Kaliua yenye thamani ya Shilingi Milioni 800 ambayo imekamilika kwa asilimia 100% kitendo ambacho kitasaidia uimalishwaji wa utoaji na utendaji wa Haki kwa Wananchi wa Kaliua.
✅ UANZISHWAJI WA HUDUMA ZA MAMLAKA YA MAPATO KALIUA(TRA)
Wananchi wameanza kupata huduma bora kutoka Mamlaka ya mapato Kaliua ambapo awali walikuwa wakihudumiwa Wilayani Urambo kitendo kilichokuwa kikiongeza gharama za maisha ikiwemo gharama za Usafiri, Maradhi, Chakula na kuwepo kwa malalamiko ya wafanyabiashara