Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machalli avamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana!

Mbunge wa Kasulu mjini Moses Machalli avamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana!

nngu007

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2010
Posts
15,860
Reaction score
5,801
JUNE 20, 2013


Mbunge wa kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mh. Moses Machalli

Habari zilizoifikia Maisha Times muda huu kutoka Dodoma zinaripoti kwamba Mbunge wa Kasulu mjini kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Moses Machalli amevamiwa na kupigwa na watu wasiojulikana katika eneo la, tukio hilo limetokea jioni hii wakati Machalli akiendesha gari lake mita kadhaa kutoka ilipo nyumba anayoishi baada ya kuwapigia honi vijana kadhaa waliokuwa wakitembea katikati ya barabara ili wasogee pembeni naye aweze kupita kitendo ambacho kilionekana kuwaudhi na kuwakera vijana hao ambao walianza kuipiga na kuigonga kwa nguvu bodi ya gari ya Machalli jambo ambalo lilimfanya Machalli kusimamisha gari na kushuka ili kujua kulikoni hali iliyopelekea vijana hao kumtolea matusi kadhaa ya nguoni na pindi machalli alipowajibu kwa hasira ndipo kipigo kikali kilipoanzia.

Shuhuda wetu aliyekuwa jirani na eneo la tukio anasema kwamba Mh. Machalli amepigwa na vijana zaidi ya nane jambo ambalo lilipelekea hata yeye kushindwa kumsaidia kwa kuhofia kuunganishwa katika kipigo.

Maisha Times itazidi kukuhabarisha zaidi kuhusiana na tukio hili kadiri habari zitakavyozidi kupatikana.

Imechapishwa na Mkamis

PIA SOMA
- Uelewa wangu juu ya kundi la watu wasiojulikana

~ Matukio ya Watu kupotea na wengine kudaiwa kutekwa, nini kinaendelea kuhusu usalama wa raia

- Kiongozi wa Madaktari (Dr. Ulimboka) atekwa, aokotwa akiwa katika hali mbaya sana
 
Juzi kamwambia nini yule mama pale bungeni ?
 
hiii ilipangwa na Maccm itokeeee, recall suara la ulopokaji bungeni
 
Machali kaadhibiwa makusudi! Hii nchi ilipofika inaelekea kusambaratika ingawa wenye dhamana wanapuuzia!
 
Watanzania usisubiri ikutokee wewe!
tumefikia pabaya!
 
Haya sasa! Hivi majuzi si kuna kauli aliitoa pale majengoni jamani?

Siyo yenye inamgharimu jamani?
Tutaona mengi sana kabla ya!
 
Hao ni green guards tu wametumwa kufanya hivyo kutokana na alivyowakamulia ndimu machoni juzi.
 
Back
Top Bottom