Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima ataka Masheikh wa Uamsho waachiwe na Sheria za uhujumu uchumi zirekebishwe

Mbunge wa Kawe Askofu Gwajima ataka Masheikh wa Uamsho waachiwe na Sheria za uhujumu uchumi zirekebishwe

Mimi siongezi neno hapa

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima amelishauri Bunge kuwa Sheria kandamizi zilizotungwa mwaka 2019 ikiwemo Sheria ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji fedha zifanyiwe Marekebisho kwani kuna Maelfu ya watu Wamebambikiwa kesi hizo mpaka sasa Wanasota Mahabusu bila kujua hatma yao.

Aidha, Gwajima amesema haoni sababu ya Masheikh wa UAMSHO kuendelea kusota Mahabusu kwa miaka 9 bila kujua hatma yao

"Kuna Masheikh wa Uamsho wapo Mahabusu mwaka wa 9 sasa, hebu imagine ni Baba yako anasota Mahabusu kwa miaka 9 bila kujua atahukumiwa lini na vipi ikibainika hawana hatia mtawalipa nini?. Simaanishi hawana hatia au wanayo nashauri ni vyema wahukumiwe wajue moja.

Arusha kuna Masheikh 64 wanasota Mahabusu kwa kesi ya Ugaidi, najiuliza hivi hii nchi Magaidi ni Masheikh tu Hakuna watu wengine"Josephat Gwajima.

Ahsante Gwajima kwa kuliona hili.
Chidi mnafiq sana
 
Hiyo hotuba ya Gwajima bungeni inamwonyesha jinsi alivyo mnafiki. Yeye ni mbunge wa kawe, na hao masheikh wa uamsho au wa arusha hawapo kawe.Na zaidi anaingilia Mambo ya mahakama.
 
Eeeh ahya vizuri kwa kuwakumbuka watumishi wa Mungu wenzie, nilitaka kusema siku zote alikuwa wapi kuyasemea hayo? Ila nimekumbuka yaliyopita si ndwele tugange yajayo.
 
Mbunge wa Jimbo la Kawe, Mchungaji Dkt. Josephat Gwajima, amesema, kuna idadi kubwa ya watu wako mahabusu kutokana na suala la utakatishaji wa fedha ambao wako waliobambikiziwa kosa hilo na watumishi wasio waaminifu wa vyombo vya dola na kuomba suala hilo liangaliwe kwa kina.

"Kuna watu wengi sana Naibu Spika wako ndani, wako mahabusu maelfu ya watu kwa sababu ya hili suala la utakatishaji fedha kubambikiziwa na watu wasio waaminifu katika vyombo vyetu vya Dola"

"Mpaka leo kwa mujibu wa takwimu kuna watu 1,701 ambao wako mahabusu kwa sababu ya ama kwa ajili ya utakatishaji fedha Money laundering au kwa sababu ya uhujumu uchumi"

"Unakuta mtu anakwenda kwa mfanyabiashara kukusanya mapato au kudai mapato au malimbikizo ya mapato anakwenda na 'charge' kabisa kwamba usiponipa fedha kadhaa tayari nina hati hii hapa nakuwekea Money laundering au nakuwekea Economic Sabotage"

"Haileti "sense" kwanini wale Masheikh wa uamsho wako ndani mpaka leo, leo ni miaka 9. Najaribu kuwaza ingekuwa mimi, Baba au ndugu yangu ambaye ambaye mpaka leo miaka 9 yupo ndani, itakuwaje baada ya miaka 20 mkagundua hawana hatia mtawalipa nini kwa miaka waliyopoteza"

"Nashangaa kwanini Masheikh tu ndio wako ndani kwa kesi za ugaidi, hakuna gaidi mwingine ambaye sio sheikh, naomba tuangalie kwa undani sana namna ya ku-handle suala hili, sisemi wana hatia au hawana hatia, sijadili kosa lao lakini basi wangehukumiwa ikajulikana"
Na inawezekana anatafuta Kiki ya kuja kugombea uraisi 2025. Na sijui ni watu wa aina gani watamuelewa kwa kauli yake hiyo ya kujitoa ufahamu.
 
Huyo mwehu anataka kwenda na upepo 🤣🤣🤣🤣
Mkristo ama Mwislamu, madam kazaliwa Tanzania, anathamani sawa na mtanzania yeyote,

Napenda Jinsi wa Marekani walivyo, Thamani ya mtu mmoja wa kimarekani akipotea/kuwawa katika nchi Fulani, ni lazima taifa Hilo lijitetee kwa nini mmarekani huyo kauwawa

Naomba siku moja tufike huko, Mtanzania yeyote bila kujali dini, rangi, kabila au Chama chake, pindi inapotokea ameonewa, uttetezi wake utokee kila pande za nchi na Kwa kila mtanzania
Bungeni, uraiani na sehemu yoyote ili mradi tu ni mtanzania na ameonewa Kweli

Gwajima, nimekuelewa sana, na huu ndio utanzania, Dini ukiwa sehemu husika umevaa na yake majoho

Tutambulike Kwa utanzania na sio Kwa dini zetu tulizonazo

Mungu Ibariki Tanzania
 
Kwani Magu ndo kawaweka mashehe ndani?
Mnamsingizia kila kitu sasa

..kama aliweza kuwatoa babu seya na papii waliolawiti watoto wa shule basi alikuwa na uwezo wa kuwatoa mashehe ambao imeshindikana kuwatia hatiani kwa miaka 6 sasa kesi iko mahakamani.
 
..kama aliweza kuwatoa babu seya na papii waliolawiti watoto wa shule basi alikuwa na uwezo wa kuwatoa mashehe ambao imeshindikana kuwatia hatiani kwa miaka 6 sasa kesi iko mahakamani.
Pengine mafaili yao yana siri nzito sana.
Kwa jinsi Magu alivyokuwa na sifa asingeweza kuacha kuwatoa
 
Pengine mafaili yao yana siri nzito sana.
Kwa jinsi Magu alivyokuwa na sifa asingeweza kuacha kuwatoa

..watolewe mahabusu.

..wakati huohuo uchunguzi dhidi yao uendelee.

..uchunguzi ukikamilika na ikionekana wana makosa wapelekwe mahakamani.
 
Hao jamaa serikali kuwashikilia bila kuwafikisha mahakamani ni kama kuwaogopa, wanaogopa sheria inaweza kuwaachia huru watu ambao ni "threat" kwenye jamii.

Aina ya mahubiri waliyokuwa wanayafanya ndio inayowagarimu, na hili limesababisha hata marais "wenzao" wasiwaachie huru. Tuliona watu wakimwagiwa tindikali bcoz of them, na walipokamatwa hali ikatulia.
Ushahidi uwapi Kama walihusika? Upeleke
 
Akifanya hivyo basi atakuwa amefanya kosa kubwa la kimkakati (kisiasa, kiulinzi, nakadhalika)

Kwa kuwaachia atawake mahali pagumu CCM Zanzibar na Hussein Mwinyi

Muungano, Utulivu, Uhuru wa wakristo wa Zanzibar navyo vitakuwa mashakani
Ukristo imeanza juzi znz? Acha roho mbaya
 
Mimi siongezi neno hapa

Mbunge wa Kawe, Josephat Gwajima amelishauri Bunge kuwa Sheria kandamizi zilizotungwa mwaka 2019 ikiwemo Sheria ya Uhujumu Uchumi na Utakatishaji fedha zifanyiwe Marekebisho kwani kuna Maelfu ya watu Wamebambikiwa kesi hizo mpaka sasa Wanasota Mahabusu bila kujua hatma yao.

Aidha, Gwajima amesema haoni sababu ya Masheikh wa UAMSHO kuendelea kusota Mahabusu kwa miaka 9 bila kujua hatma yao

"Kuna Masheikh wa Uamsho wapo Mahabusu mwaka wa 9 sasa, hebu imagine ni Baba yako anasota Mahabusu kwa miaka 9 bila kujua atahukumiwa lini na vipi ikibainika hawana hatia mtawalipa nini?. Simaanishi hawana hatia au wanayo nashauri ni vyema wahukumiwe wajue moja.

Arusha kuna Masheikh 64 wanasota Mahabusu kwa kesi ya Ugaidi, najiuliza hivi hii nchi Magaidi ni Masheikh tu Hakuna watu wengine"Josephat Gwajima.

Ahsante Gwajima kwa kuliona hili.
Huyo Gwajima hawajui hao, aende Msumbiji akaone wanachofanya wafuasi wao
 
Back
Top Bottom