#COVID19 Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima asema kutokufanya social distancing wakati huu wa Covid-19 ni msimamo sahihi

#COVID19 Mbunge wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima asema kutokufanya social distancing wakati huu wa Covid-19 ni msimamo sahihi

Behaviourist

JF-Expert Member
Joined
Apr 8, 2016
Posts
39,926
Reaction score
95,626
Wakatia akichangia hoja Bungeni, leo tarehe 10 Februari, 2021, Mbunge huyo wa Jimbo la Kawe amesema:

"Kuna ugonjwa wa Covid-19 ambao umetikisa dunia na nchi yetu imechukua msimamo tofauti na nchi nyingine zozote.

Waheshimiwa Wabunge, natumia nafasi hii kuwatia moyo. Msiogope. Msiogope mnapoambiwa kwamba kuna phase ya pili ya Covid-19. Kilicho na nguvu nyuma ya Covid-19 ni woga uliotengenezwa juu ya Covid-19. The fear of Covid-19 is even [more] powerful than Covid-19 itself (Woga wa Covid-19 una nguvu zaidi ya ugonjwa wenyewe)

Watanzania wote na watu wote, tushinde woga. Tusiogope, tumeshinda na tusonge mbele. Na msimamo wetu wa kutokuchanjwa na msimamo wetu wa kutokufanya social distancing ni msimamo sahihi na utatufikisha mahala sahihi."


Hivi mtu kama huyu anaweza akawa ana akili timamu?
 
Huyu ni brainless na kisomoless kabisa! Yaani mawakala wa kifo wanajitanabaisha waziwazi na huenda ameshawanyonya waumini wake vya kutosha na hahitaji zaka na sadaka zao Tena!

Yaani anajiita askofu huku akishindana na sayansi ambayo haijawahi kutoa majibu yasiyo sahihi! Ngoja nimuombee kwa Mungu wa kweli na haki ninayemuamini ili amchape nao kidogo some ulivyo mtamu na ikibidi aondoke nao! Tenda muujiza Mungu mtakatifu!
 
Back
Top Bottom