Mbunge wa Kilombero, Abubakar Assenga amemuomba Rais Samia Suluhu Hassan kutazama upya bei ya ushuru wa mazao jimboni humo na kutozuia uvuvi wa samaki aina ya mlamukaliandili, ili kuondoa kero kwa wananchi.Assenga amesema hayo leo Jumatatu Agosti 5, 2024 katika mkutano wa hadhara ambao Rais Samia alizungumza na wananchi wa Ifakara katika Uwanja wa CCM Ifakara mkoani Morogoro.
Hapa bei ya mpunga sasa hivi ni ndogo, gunia ni Sh80,000 nasema uongo? Na ile tozo ya ushuru geti la Idoto ni tatizo, uongo, kweli? Kama tozo ni asilimia tatu, sisi hatukatai kulipa, asipotoshe Mheshimiwa Rais.