Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ataka matokeo ya Urais yahojiwe Mahakamani

Naomba wanasheria mnisaidie hivi walio andika katiba yetu walitoa sababu zipi za matokeo ya urais kutopingwa mahakamani?

Hili swali linaniumiza kichwa maana naona wazi kipengele hiki kinaenda kuiletea nchi matatizo hapo baadae.
Hii ni Katiba ya mwaka 1977 toleo la mwaka 2000 ambalo inabidi lisomwe pamoja na Sheria ya vyama vingi ya mwaka 1992 pamoja na marekebisho yaliyofuata.

Wakati wa JK Nyerere Katiba ilikuwa inaandikwa na Jopo la wateule wake. Nahisi jopo la mwisho Pius Msekwa na Kingunge Ngombale Mwiru (RIP) walikuwa wajumbe. Yawezekana kwa mazingira ya wakati ule haikuonekana sababu ya ku-challenge matokeo Mahakamani kutokana na uchanga wa Taifa. Mwaka 1977 Watanzania walikuwa Milioni 16 tu na kiwango cha elimu kilikuwa kidogo sana.

Ila kwa wakati huu Tume Huru, Ku-challenge matokeo Mahakamani ni vitu vya lazima kutokana na mabadiliko ya kisiasa, ki-demografia na kielimu. Yote haya yalipaswa kuwa kwenye katiba Mpya ambayo kwa uzembe na udhaifu wake Jakaya Kikwete alishindwa kuimaliza. Na huyu Jiwe anatumia udhaifu wa katiba ya mwaka 1977 kujifanya DIKTETA. Kwa kweli dhambi ambayo Jakaya Kikwete hawezi kusamehewa ni kutumia Mabilioni ya Shilingi za walipa kodi za waTanzania kuondoka madarakani bila kuleta Katiba Mpya.
 
Kama ni kikao cha siri we hii habari uliipataje? Mbona unapenda kupotosha potosha! Mmekosa sehemu ya kupapasa kabisa?
Wakati kikao cha siri kikiisha si wabunge wanatawanyika na apo ndo wazalendo wanapata habari za kikao cha siri
 
Hivi mbona sijawahi kusikia Mh.Sugu akihoji Mbowe kukaa sana madarakani kama Mwenyekiti wa Chadema? Na je, ingetokea Mbowe akawa Rais angeweza kuhoji au anahoji kwasababu Chadema haijashika madaraka? Sugu anatuzuga tu.
 
Nipo kwenye basi la Sauli naelekea Mbeya, nani mwenyeji huko tuonane? Nitalala pale Appieline Hotel. Floor ya kwanza room no.112. Karibuni tuonane
 
Hongera Sugu. Wote tudani na kudai na kudai bila kuchoka:. Katiba Mpya, Tume huru ya uchaguzi na kuhoji matokeo ya Uraisi mahakamani.....
Wakati wa uchaguzi kura zote zikiwemo za raisi zihesabiwe na kubandikwa vituoni
Wanahangaika na katiba mpya ya taifa wakati wameacha katiba ya Chadema inayomuacha Mkiti akae madarakani bila kikomo sijui hawajaisoma bado?
 
Isingekuwa uzembe na udhaifu wa Jakaya Kikwete mwaka 2015 wakati wa mchakato wa Rasimu ya Katiba Mpya, haya maswali ya akina Sugu yasingekuwapo.

Ni nini kilimpata JK mpaka akashindwa kumalizia Katiba ya Wananchi?
Nafikiri ukimuuliza mzee Warioba ndio analo jibu sahihi,nini kilifanyika.
 
Nipo kwenye basi la Sauli naelekea Mbeya, nani mwenyeji huko tuonane? Nitalala pale Appieline Hotel. Floor ya kwanza room no.112. Karibuni tuonane
😆😆😆😆
 
Hotuba zake za mwisho mwisho Bungeni.
 
Ukitaka kuwaumiza CCM wewe ongelea Tume Huru pamoja na mabadiliko kama haya - aisee !!
 
Nafikiri ukimuuliza mzee Warioba ndio analo jibu sahihi,nini kilifanyika.
Nayeye Mze wa watu atakwambaia hajui kilichotokea labda tu tuwe wavumilivu kama tulivyo sisi wa Tz kila jambo kwetu ni mchakato, mchakato mpaka mchakato ndo action p'se. After all watengenezaji walikuwa wajanja hawakujipa timeframe.
 
Kwani Sugu alipata ushindi kwenye tume gani? Hahahahaha

Sent from my iPhone using Tapatalk
Hapo na mimi ndo nashangaa. 2015 wabunge wengi UKAWA walipita na tume hiyo hiyo ikawapitisha sasa leo wanaigeuka kweli wanadamu hatuna shukrani.
 
Kwani Sugu alipata ushindi kwenye tume gani? Hahahahaha

Sent from my iPhone using Tapatalk
Ndio ushaambiwa hadi roho ya kiumbe mwenzio ilitoka, undondocha mwingine unakera..au unajifanya kama vile alitangazwa kirahisi kama mlivyofuta matokeo ya Zanzibar??
 
si kwamba hawajui , wameamua kujitoa akili tu .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…