sawa kabisa! kuna wakati tunaweza kuwa na wasiwasi na vyombo vyetu lakini mara nyingi nimekuwa nikiamini sana Mahakama Kuu na ya Rufaa katika mambo mengi kuliko mahakama nyingi za chini. Na upande mmoja ni kuwa wapo majaji na mahakimu ambao bado wanaangalia ushahidi na wanaofuata kokote utakakowapeleka.
Kuna kila dalili kwamba mbunge wa Mwibara kwa tiketi ya CCM bwana Kajege atavuliwa kiti chake cha ubunge punde. Taarifa zaidi zitawajia.
wako slow.. habari zinakuja JF kwanza wengine wanafuata!!! we taste the food before it is taken to the table!
wako slow.. habari zinakuja JF kwanza wengine wanafuata!!! we taste the food before it is taken to the table!
Huyu JAJI naona anafaa kukabidhiwa faili zoote za kesi za kupinga matokeo ya ubunge, coz ndani ya Bongo kushinda kesi ya matokeo mahakamani tena ikiwa mlalamikaji mpinzani, sio mchezo babake!
Tumeona JAJI wengi hapa ukereketwa mbele sheria baadae.
KLHNews said:mshitakiwa alitoa vitu mbalimbali vikiwemo kanga, vitenge, chumvi na miche ya sabuni aina ya kanga pamoja na fedha taslimu, kila mwanamke sh 500!
Usimpe jaji credit kwa maamuzi yanayokufurahisha; kumbuka kuna pande mbili za kesi, siku zote anayeshinda hufurahi, siku akishindwa basi jaji anakuwa mla rushwa...jaji huyu huyu anaweza kutoa maamuzi mengine kesho ambayo kwa mujibu wa sheria ni sahihi ukamchukia vibaya; wapo watu kwa maamuzi haya wanataka hata kumnyonga
..... Sawa kabisa, Sheria ni Msumeno... au siyo 😉
of course, mwendapole that is the nature of the game.. refa akiamua goli lenu linakubalika mnashangilia, akimezea kuzidi kwa adui yenu akasawazisha mnaweza kumkwida.
Mwendapole, kinachotokea hapa ni kwamba watu wameichoka sana CCM kiasi kwamba kila jambo baya linalowapata watu hawana budi kushangilia. Ndio maana unaona hapa tunashangilia, wakati yule mbunge wa TLP kule Biharamulo yalipoenguliwa matokeo yake wengi wetu hapa tulisikitika sana tena sana. Kwa maana nyingine ni kwamba watu wengi hapa ni wanachama wa upinzani kwa kadi au bila kadi, which is very much encouraging maana watu wapo ready for change anytime the environment is ripe. Ni hivyo tu kaka.
Dah, huyu bwana mdogo ameenguliwa?
Aisee, niliosoma na kijana huyu akiwa madarasa matatu nyuma yangu huko shule ya msingi na baadaye tukakutana pale Tabora akiwa pale Kazima wakati mimi namalizia form 6. Alikuwa mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu kwenye timu ya UMISETA. Ninaambaiwa kuwa alipewa kazi pale Mambo ya Nje kwa kuunganishiwa na wazee wa timu ya Asante Tololo mara tu baada ya kumaliza form 6 pale Azania kusudi aichezee timu hiyo. Nadhani baada ya dhahama hili, atatulia na kutafakari jambo la maana analoweza kuifanyia jamii nili kuachana na siasa za kibabaishaji namna hii zinazoweza kumchafulia jina katika jamii. Badala ya kuwa mtetezi wa ufisadi, asimame kuwa mtetezi wa maslahi ya nchi. Jambo zuri ni kwamba alitumia nafasi yake pale mambo ya nje kujiendeleza sana ki-elimu kwa hiyo ninadhani hatakosa jambo la maana la kufanya.