Dah, huyu bwana mdogo ameenguliwa?
Aisee, niliosoma na kijana huyu akiwa madarasa matatu nyuma yangu huko shule ya msingi na baadaye tukakutana pale Tabora akiwa pale Kazima wakati mimi namalizia form 6. Alikuwa mchezaji mzuri sana wa mpira wa miguu kwenye timu ya UMISETA. Ninaambaiwa kuwa alipewa kazi pale Mambo ya Nje kwa kuunganishiwa na wazee wa timu ya Asante Tololo mara tu baada ya kumaliza form 6 pale Azania kusudi aichezee timu hiyo. Nadhani baada ya dhahama hili, atatulia na kutafakari jambo la maana analoweza kuifanyia jamii nili kuachana na siasa za kibabaishaji namna hii zinazoweza kumchafulia jina katika jamii. Badala ya kuwa mtetezi wa ufisadi, asimame kuwa mtetezi wa maslahi ya nchi. Jambo zuri ni kwamba alitumia nafasi yake pale mambo ya nje kujiendeleza sana ki-elimu kwa hiyo ninadhani hatakosa jambo la maana la kufanya.