Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

Hawa jamaa wasije kucheza mchezo kwamba wapoteze Mwibara na kumuua Slaa maana CCM ya JK bwana mazingaombwe matupu .

I don't think so.

Kesi dhidi ya Slaa ni dhaifu sana. Kama upande wa mashtaka unaleta mashahidi wanaojikanyanga wenyewe ni dhahiri kuwa hawwana kesi thabiti.
 
Duh, Haya haya jambo limezua jambo!

Nakumbuka huyu Mbunge Mutamwega Mgaywa wa TLP kabla ya kuachia ubunge alijitolea kiinua mgongo chake kitu kama millioni 30 na upupu kwa wananchi wa Mwibara. Niliposikia matokeo kusema kweli nilisikitika sana kwani huyu katoa fedha zake kuingia ktk mfuko wa maendeleo ya wilaya lakini wananchi wakamchagua yule alotoa Pilau, T shirt na kofia..
Mungu ashukuriwe! ni mwanzo mzuri huu kuna kila haja ya kumpongeza jaji huyu na wananchi wa Mwibara yaani nimefurahi kuona mapinduzi yameanza toka nyumbani.
 
Ninapenda kumtumia salam za pole, My brother Charles, ingawa pia sisikitiki sana maana kijana alishafikia hatua ya kujiona amemaliza dunia kwa kupata ubunge tu, yaani kwa kifupi masikio yake yalishaanza kukipita kichwa chake! Na kama nilivyosema jana, ni pale bin-adam anapofikiri amesimama ndipo huanguka! puh! chali!

Ubunge, au cheo chochote ni dhamana tu na sio a right, kama kijana alivyokuwa ameanza kuamini kutokana na matendo yake, ninakumbuka alipokuwa anajaribu kujiweka sawa kugombea, ilibidi nimpatie card ya sherehe moja nzito ya kitaifa ili kumpa nafasi ya kukutana na kujitambulisha kwa the political heavyweights na kujiweka sawa kuweza kupitishwa kugombea ubunge na cc iliyofanyika kule Dodoma, ninakumbuka kesi yake ilipotajwa mara ya kwanza, tulifikiri kuwa anaonewa na tulikuwa tayari kumsaidia kwa hali na mali, binafsi I gave him a big hand mwanzoni bila ya kujua kuwa he would turn to be an arrogant individual and politician, akiamini kuwa he knows it all, kwa hiyo this ya kushindwa now ni a perfect Chritmas gift, na haikuwa bahati mbaya, nafikiri ni about a month ago, ndipo kijana alipogundua kuwa he is in big trouble na kwamba kesi inakuja kwa kasi mbaya sana, akajaribu kila njia behind the scene ku-reach out msaada, na hasa hakimu wa hiyo kesi, lakini the question kwa aliokuwa akiwaomba msaada ilikuwa if it was worhty kumsaidia? Wengi waliamua it was not! Na ninamuomnba asimlaumu mtu yoyote zaidi yake yeye mwenyewe!

Now let me say this, kwake mkuu Charles, najua alikuwa hajui vizuri kuwa CCM haipendi mbunge mwenye kesi, na hasa akiwa arrogant kama alivyokuwa recently, CCM cares for the number yao ya viti vingi bungeni, CCM walishafanya research kama kawaida na kujua kuwa hawezi kushinda hiyo kesi, na pia I have bad news kwake kuwa hata uchaguzi utakaporudiwa CCM hawatampa nafasi tena ya kugombea, labda abadilishe chama cha siasa, Hussein mikono yake sasa imejaa, anatafuta urais kwa hiyo hawezi tena kumsaida hasa baada ya u-arrogant alio uonyesha, kwa maneno mengine ni kwamba the brother is done no help!

CCM sasa wana kazi ya kugombea viti vitatu kwenye uchaguzi mdogo ujao, yaani majimbo ya Kiteto, Biharamulo, na hili sasa la Mwibara, sasa hii ni kazi ya Msekwa, Makamu mstaafu hayupo tena na kama alivyoahidi siku ya kustaafu kwake kuwa hana mpango wa kucheza siasa za remote control, na mimi binafsi ningemshauri kuwa baada ya miaka 15 ya umakamu na kukomboa a record ya viti vya ubunge 26, Why take a risk ya kuharibu his record now? Maana najua for a fact kuwa Biharamulo is out of reach, tena no way!

Kwake bwana Charles, I hope sasa utakuwa ni wakati muafaka wa kutafakari yaliyojiri na kujiweka sawa kwa the future, still young, na kwa sababu ni msomi pia wa uchumi tena aliyebobea basi kushindwa ubunge sio mwisho wa maisha, isipokuwa tu politically anayo a very big task kuweza ku-make a come back, kwa sababu sio rahisi kuyarudia madaraja alioyabomoa yeye mwenyewe na his arrogancy, on his way up! Kweli power corrupts!
 
Field Marshal ES,

Yaani umemsema huyu jamaa kama katoto vile, simfahamu, lakini ulivyomwelezea huruma inaniingia tayari!
 
Mkuu wangu Kithuku,

Huu ni uwanja wa kumkoma nyani giladi, huwa hatuna peremende hapa, huyu mbunge aliyeshindwa ni kijana, na wewe unajua jinsi Tanzania ambavyo tumekuwa tukililia viongozi vijana, sasa ishu kama ya huyu kijana ndio inaua kabisa ile hoja ya vijana na uongozi wa taifa letu, na kutuumiza mimi na wewe huko mbele ya safari, sasa hatuwezi kuja hapa na kudanganyana, especially kijana anapoharibu!

Na kama tulivyoahidi hapa ni kumkoma nyani tu, bila kumuangalia usoni! Mimi huwa sina huruma na kiongozi anapoangushwa na arrogancy zake mwenyewe, ila nina huruma na taifa letu na walalahoi wake!
 
FMSE political newcomers wanahitajika sana matatizo yao ndo hayo ya kupandisha mabega na vichwa kuvimba, Mutamwega alikuwa chachu muhimu bungeni. Jamani tupigeni kampeni na kushinda kihalali huu ujanja ujanja na siasa za kishamba hazitufikishi popote.
 
Duh, Haya haya jambo limezua jambo!

Nakumbuka huyu Mbunge Mutamwega Mgaywa wa TLP kabla ya kuachia ubunge alijitolea kiinua mgongo chake kitu kama millioni 30 na upupu kwa wananchi wa Mwibara. Niliposikia matokeo kusema kweli nilisikitika sana kwani huyu katoa fedha zake kuingia ktk mfuko wa maendeleo ya wilaya lakini wananchi wakamchagua yule alotoa Pilau, T shirt na kofia..
Mungu ashukuriwe! ni mwanzo mzuri huu kuna kila haja ya kumpongeza jaji huyu na wananchi wa Mwibara yaani nimefurahi kuona mapinduzi yameanza toka nyumbani.[/QUOTE]

Hii imenikumbusha ni jinsi gani huo uchaguzi ulikuwa umechafuliwa na takrima ikiongoza.
Nilifanikiwa kuongea na watu mbalimbali kijijini kwangu ambao walishiriki ktk uchaguzi. Bahati mbaya binafsi sikubahatika kushiriki.Nililenga zaidi kudadisi kundi la wazee na akina mama wa pale kijijini.

Walichoniambia majority ni kwamba wao walikuwa hawaangalii sera au utashi wa mgombea. Walitoa kura kwa yule aliyetoa takrima zaidi. Hivyo aliyewanunulia pombe (gongo ikiongoza) zaidi kwa akina baba, na aliyegawa vitu kama kanga na pesa ya kama kilo moja ya sukari kwa akina mama ndiye alionekana kuwa kiongozi anayewafaa zaidi.

Walinipa black n white kwamba hawakuwa tayari kutoa kura kwa mtu asiye na kitu au ambaye hakuwa tayari kutoa kitu kidogo.

Nakawauliza je? na ahadi zinazotelewa?. Wakaniambia hawamind sana maana miaka nenda rudi wameahidiwa mengi lakini hawaoni utekelezaji wake.Wamekata tamaa.

Nikajiuliza, mind-set kama hii inatupeleka wapi kama taifa? Je inawezekani kuibadili? Maana kwa maneno mengine ni kwamba wale watu wa kijijini wamechukulia matatizo kama sehemu ya maisha ya kila siku.

Wamekata tamaa kuangalia future.Wanachohitaji at present ni mkono uende kinywani tuu, ya kesho ni majaliwa.

Na hapo ndipo wanasiasa wachafu wanapowapatia hawa wazee wakati wa uchaguzi-wananunua pombe, wanapika ubwabwa,wanapeleka kanga, kofia,sabuni na kuwapa cash TZS 500.

Ndugu zangu,kitu takrima alichokuwa anang'ang'ania Mkapa ni kitu kibaya sana. Madhara yake limekuwa janga la kitaifa.
 
Msema kweli ni kipenzi cha Mungu, hili limenigusa mimi binafsi Charles ni mtu wangu wa karibu sana nimehuzunika sana kwa wengi humu hukumu inakuwa ya haki inakwenda upande wa wapinzani na mahakama kuu na rufaa tunakuwa na "imani" nazo.

Hao hao wakitengua matokeo ya Karatu watakuwa "waonevu"....
 
Jamani mlioko Dar hebu msaidie Mutamwenga wakati wa kampeni ukifika, huyu jamaa yupo serious sana. Ni wabunge wachache waliokuwa wamejichimbia huko majimboni mwao, sema ndio hivyo tena wananchi wetu wamekata tamaa, isingekuwa kuwa rahisi katika hali ya kawaida kumshinda Mutamwega kwa ajili alivyojitoa kule
 
Mkuu wangu Kithuku,

Huu ni uwanja wa kumkoma nyani giladi, huwa hatuna peremende hapa, huyu mbunge aliyeshindwa ni kijana, na wewe unajua jinsi Tanzania ambavyo tumekuwa tukililia viongozi vijana, sasa ishu kama ya huyu kijana ndio inaua kabisa ile hoja ya vijana na uongozi wa taifa letu, na kutuumiza mimi na wewe huko mbele ya safari, sasa hatuwezi kuja hapa na kudanganyana, especially kijana anapoharibu!

Na kama tulivyoahidi hapa ni kumkoma nyani tu, bila kumuangalia usoni! Mimi huwa sina huruma na kiongozi anapoangushwa na arrogancy zake mwenyewe, ila nina huruma na taifa letu na walalahoi wake!

Mkuu ES,

Naona umeongea mengi kweli kweli. Lakini wengine ni Wambeya na tunataka zaidi, kama unaweza tuongezee juu ya huyu mwenzetu amefanya nini mpaka panga la FMES limlime hivyo?
 
Mkuu siwezi kusema yote, ila kama Masatu, nimesikitishwa sana maana I spent a lot of time na kijana, pale Garden
City kwa kushirikiana na the Mahendes kutafuta njia za kumfanya aweze kupitishwa na cc,

Na toka alipokuwa anamalizia MA yake kule Florida, ambako alijisomesha mwenyewe kwa hela zake, kuna wakati mambo yalikuwa magumu sana financially kwake, mpaka kumukutanisha na Muungwana ili apewe msaaada na wizara ya nje,

Sasa for him to turn out of what he became recently, ilikuwa ni huzuni kubwa sana kwangu, na kama kawaida huwa ninaanza kusikia kutoka kwa wengine, ndugu yangu it takes a lot mpaka kushindwa mahakamani ukiwa mbunge wa CCM!

anyways mkuu Mtanzania, ninatakutafuta kwenye private baadaye!
 
Masatu, huyu Muguta mimi nilisoma naye pale Namibu na baadaye nikakutana naye Tabora wakati namalizia form 6 yeye akiwa form 2 au form 3 pale Kazima. Taarifa nilizopata kutoka kwa watu mbalimbali zinaonyesha kuwa kweli tangu ndugu Muguta awe Mbunge alikosa dira ya kisiasa. Unajua kazi za siasa zinataka unyenyekevu sana kwa wananchi na washirika, lakini sidhani kama alifanikiwa hilo kulingana na maneno ya wengi ninaoongea nao huko Mwibara. Nina kila sababu ya kukubaliana na maneno ya FMES ingawa sina uthibitisho nayo. Alisaidiwa sana kupata ubunge tangu kwenye mchakato wa primaries; haikuwa rahisi kwake kumshinda Mtamwega. Lakini yeye baada ya kuwa mbunge aliwapiga teke wote wale waliomsaidia, na hata waliomchagua pia aliwapiga teke. Huwezi kuwa mwanasiasa katika staili ya namna hiyo.
 
Kichuguu,
Mzee wangu kumbe tumesoma shule moja!....tofauti nadhani ni miaka tu... pale Kibara mzee wangu kwetu ilikuwa barabara ya Musoma ubavuni kwa na yule msukuma mwenye mbwa wengiii ukielekea uwanja wa Mpira kwa mzee Husseni Machumu hapo ndio home nilipokulia!.
 
Mkuu Bob,

Kile kiwanda cha siagi bado kipo au vipi, maana enzi zile nilikuwa nikizibeba sana na Air Tanzania, na kuwauzia wahindi Dar na hasa Bahkressa, au ndio siasa zetu kilishakufa?
 
Duh, hata wewe ulikuwa mitaa hiyo?.... yes ama kweli dunia ndogo sana. Sijafika mitaa hiyo toka mwaka 1995 unajua tena wazee wanatoka kisiwani.
 
Mkuu Bob,

Kile kiwanda cha siagi bado kipo au vipi, maana enzi zile nilikuwa nikizibeba sana na Air Tanzania, na kuwauzia wahindi Dar na hasa Bahkressa, au ndio siasa zetu kilishakufa?

Kumbe tupo wengi hapa. Mimi nilitoka huko tangu mwaka 1971, wengi wa wanachi wetu Tanzania walikuwa hawajazaliwa!!
 
duh nilidhania mwenye mvi mimi peke yangu... kumbe ndiyo vijana wa "siasa ni kilimo" eh.. na "miaka kumi baadaye"...
 
Sijui Hata Ndg Charles Alisahau Hata Zile Takrima Alizopata Toka Kwa Bunda Bus Zakusaidia Kampeni Zake Kwani Kibara Ilikuwa Haiko Tayari Kusikiliza Anachosema Lakini Watu Kama Bunda Bus Services Wanaheshimika Walimpa Shavu. Ila Mtamwega Mtoto Wa Mjini Usishangae Akachukue Tiketi Hiyo Kupitia Ccm Ili Ajihakikishie Ushindi Mapema
 
Mambo yamejala mu mkambo.Hivi ndivyo demokrasia inavyokuwa hasa unapokuwa na miimili iliyohuru.Si maanishi kwakuondolewa mbunge wa chama Tawala tu,la hasha ata kama angekuwa mpinzani haki inatakiwa itendeke.
 
Kajege alishinda kesi... hivi uchaguzi utafanyika tena au ndio kapewa kiti au ndio asubiri mwakani?
 
Back
Top Bottom