Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

Mbunge wa Mwibara (CCM) apoteza kiti

sawa kabisa! kuna wakati tunaweza kuwa na wasiwasi na vyombo vyetu lakini mara nyingi nimekuwa nikiamini sana Mahakama Kuu na ya Rufaa katika mambo mengi kuliko mahakama nyingi za chini. Na upande mmoja ni kuwa wapo majaji na mahakimu ambao bado wanaangalia ushahidi na wanaofuata kokote utakakowapeleka.

Vipi aliyemwachia Zombe??
 
ccm wajanja sana. wamevuuuuuuuuuuutaaaaaaa kesi weeeeeeeeeeeee hadi miaka imeisha ndo wanatoa hukumu. msijidanganye hapo hakuna uchaguzi mdogo tena kwani muda hautoshi. kajege keshalamba maposho yake mawilimawili mpaka basi! sasa atarudi nayo tena kugawa t-shirt aendeleze ushindi wa kisindo mwakani!!!!!!!!!!

hii ndiyo bongo bwana

na huyu jaji ni bonge la msanii hadi kamridhisha mzee mwanakijiji! ndiyo kamkuna mzee ambaye anajinadi kuwa "upset and tired"

msijidanganye yule jaji alikuwa pale kuhakikisha maslahi ya ccm yanalindwa. ccm ndiyo yenye dola bwana, na dola ni mahakama, serikali na bunge! mpo mpaka hapo?

aliyeshinda ataishia kunawa, chakula chote wamekula wenzie na sasa wanakusanya vyombo mezani !!!!!!!!!!!

dah, bonge la demokrasia!!!!!!!
 
Hii habari ya lini? I am missing something....naomba mwongozo!
 
well done tunataka majaji wa namna hii hatutaki majaji wababaishaji wenye kuweka itikadi za kisiasa mbele kuliko maslahi ya taifa kwanza,je nijuzeni uchaguzi utarudiwa au muda umekwisha mpaka tusubiri mwakani katika uchaguzi mkuu,mwenye data naomba mnisaidie wanandugu wa jf.
 
Usimpe jaji credit kwa maamuzi yanayokufurahisha; kumbuka kuna pande mbili za kesi, siku zote anayeshinda hufurahi, siku akishindwa basi jaji anakuwa mla rushwa...jaji huyu huyu anaweza kutoa maamuzi mengine kesho ambayo kwa mujibu wa sheria ni sahihi ukamchukia vibaya; wapo watu kwa maamuzi haya wanataka hata kumnyonga

Jaji akitoa maamuzi ambayo leo yanafurahisha next time akitoa maamuzi ambayo hayafurahishi, tutamwelewa. kwanini kwa majaji wengine wanatoa maamuzi ambayo kila siku hayafurahishi. Hapo sheria iko wapi?
 
Back
Top Bottom