TANZIA Mbunge wa Newala Vijijini, Ajali Rashid akutwa amefariki katika Gesti ya Mingoyo

TANZIA Mbunge wa Newala Vijijini, Ajali Rashid akutwa amefariki katika Gesti ya Mingoyo

R.I.P mzee Akbar,ingawa hatukufahamiana sana ila kwa mda mfupi niliokujua ulikua mtu mwema sana,mchangamfu,nakumbuka tulipokua tunaongea ukiongea kuhusu hali ya nchi kwa awamu ya tano,ulikua unaongea as if kama upo upinzani kumbe ni ccm mwenzao.
Mara ya mwisho tunatoka Mtwara tukielekea mnazi mmoja kwenye lodge yako kumbe ndo nilikua nakuaga hvo.
poleni wafiwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbunge wa Newala vijijini, AJALI RASHIDI AKBAR amekutwa amefariki katika gesti ya Mingoyo - Mnazi Mmoja - Lindi, inaelezwa kuwa yeye ndio mmiliki wa gesti hiyo mpaka sasa bado chanzo cha kifo chake hakijafahamika na mwili wake umepelekwa hospitali ya Sokoine kwa uchunguzi.

Spika wa Bunge la Tanzania, Job Ndugai, ameeleza kusikitishwa kwa taarifa za kifo cha Mbunge wa Newala Vijijini, Rashid Akbar, kilichotokea leo Januari 15, 2020 mkoani Lindi, na kueleza ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia watatoa taarifa ya mazishi ya Mbunge huyo.

Wakati akiwa hai akichangia mjadala Bungeni
View attachment 1324208
Mi-ccm uchaguzi ukishafika many more will die.
 
RIP Mh. Ajali Rashid Akbar.

Mambo aliyoyafanya ktk uhai wake kama mbunge :

12 Jun 2019
Mbunge wa Newala vijijini Mh.Rashid Akbar atoa sifa hizi kwa Rais Magufuli na kuwatia mkwara wagombea pinzani katika jimbo lake. Ujenzi wa chuo na shule. Kuna shule za sekondari 20 jimboni hivyo mbunge ana visheni chuo cha VETA ili ufundi standi upatikane vijana wanaomaliza chuo wajiajiri. Vijiji vyote 142 jimboni lazima kupata umeme wa REA ili viwanda vidogo na kati vifunguliwe na vijana maana ni vijiji 30 tu ndiyo vimeunganishwa kupitia mradi wa REA Phase II.


Source : DarMpya TV
 
Januaru 15, 2020

Daktari - Marehemu alikuwa na matatizo ya moyo

Kaimu Daktari mfawidhi hospitali ya Sokoine mjini Lindi, Tanzania. Athibitisha mwili wa marehemu Mh. Ajali Rashid Akbar aliyekuwa mbunge wa Newala kupitia CCM umefikishwa hospitalini Sokoine.

Daktari mfawidhi aelezea historia ya afya ya marehemu ambaye alikuwa na maradhi ya moyo na pia kutembea na mashine maalum ndani ya mwili kusaidia moyo wake kufanya kazi vizuri.

Wiki mbili zilizopita marehemu alikuwa akipatiwa matibabu ktk Hospital ya Taifa ya Rufaa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam. Marehemu pia alikuwa akitumia dawa za kukabiliana na matatizo ya moyo ambazo zilikutwa ktk hoteli yake.

Kwa taarifa hiyo, Kaimu daktari mfawidhi wa hospitali ya Rufaa ya Mkoa Sokoine mjini Lindi pamoja na uchunguzi wa awali wa Polisi mbele ya ndugu, wamejiridhisha marehemu amefariki kutokana na matatizo ya kiafya aliyokuwa nayo.



Source: Mashujaa TV

Roving Journalist Moderator
 
Back
Top Bottom