DodomaTZ
Senior Member
- May 20, 2022
- 197
- 233
Akielezea uwepo wake Tanzania, amesema amefarijika kuwepo nchini na kwamba amepata nafasi ya kutemebelea sehemu togauti ikiwemo sehemu za fukwe, mbuga za Wanyama, Zanzibar, kukutana na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa.
Anaelezea “Umekuwa wakati mzuri kwangu, nimejifunza mambo mengi na kufurahia wakati wangu kuwepo Tanzania, nawashauri watu wengine Duniani wakipata nafasi watembelee nchi hii kwa kuwa ina vivutio vingi.”
Akielezea upande wake, Eric Shigongo ametumia ukurasa wake wa Instagram kuelezea ujumbe huo:
Nimefurahi kupata nafasi ya kumualika Mbunge wa nchini Norway, Himanshu Gulati, kutembelea Tanzania ili ajionee kwa macho yake vivutio vya kipekee vya utalii ambavyo Taifa letu limebarikiwa kuwa navyo.
Katika ziara hiyo, tulitembelea Serengeti National Park, Ngorongoro Conservation Area na baadaye kuelekea Zanzibar, ambako alipata fursa ya kushuhudia uzuri wa mazingira yetu, wanyamapori na urithi wa kipekee unaoifanya Tanzania kuwa miongoni mwa maeneo bora ya utalii duniani.
Nimefarijika kuona mgeni wangu akivutiwa na uzuri wa Tanzania pamoja na kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa katika kuhifadhi rasilimali hizi muhimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho.
Mbali na kutembelea vivutio vya utalii, alipata pia nafasi ya kukutana na Spika wa Bunge la Tanzania, Mussa Azzan Zungu, kwa mazungumzo yaliyojikita katika kuimarisha ushirikiano na uhusiano kati ya Tanzania na Norway.
Baada ya kumaliza ziara yake Tanzania Bara, aliendelea na safari yake Zanzibar kuendelea kujionea uzuri wa visiwa hivyo maarufu duniani.