Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya(CHADEMA) ajiuzulu Ubunge na kujivua uanachama, ahamia CCM

Mmh! Umesema serikali hii imeshindwa kutekeleza BAADHI ya ahadi zake. Umetumia neno BAADHI maana yake ni kwamba zipo ahadi zingine tayari ZIMETEKELEZWA.

Na yapo mengine hayakua kwenye ahadi lakini yametekelezwa.
Sasa apo shida iko wapi Wakati muda bado upo.
Acheni siasa za upotoshaji

Sent from my TECNO S1 using JamiiForums mobile app
 
Hamna haja ya uchaguzi jimboni kwake apewe tu ubunge WA ccm,aende bungeni,uchaguzi WA dharuma na kuuwa watu it's not fair..
Jiwe Mungu anamwona na ushetani wake,maendeleo hayaletwi na chama Bali na mifumo madhubuti na kila mtu!!!
 

Umeongea yote mkuu na yote ni ukweli mtupu

Nacho kiona kwa hawa hama hama ni kunusuru matumbo yao tu na kwa kufikiria labda 2020 hawataweza rudi bungeni na kwa mtizamo wao wanahisi aina ya siasa tuliyonayo haitawapa uwezo wa kurudi mjengoni wakiwa kambi ya upinzani na ili kuendelea ‘kula’ na kupata hizo ‘hadhi’ ktk jamii na sijui kusema wanaunga mkono juhudi ni aina tu ya nitoke vipi lakini hakuna mantiki kama wanavyotaka tuwaamini kwa sababu hiyo ni waoga tu na wameshindwa ku i ‘challenge’ systems na mapungufu yake yote haya

Kwa ufupi ni njaa na tumbo lkn hii ndio Africa ( katiba mama inaandikwa kwa kunufaisha kundi fulani badala ya vizazi na vizazi ktk jamhuri husika)

Natambua katiba ina ruhusu huu mchezo mchafu wa hawa hama hama lkn tunaweza kuwa watu wenye kufikiri sawa tukirekebisha hizi ‘loopholes’ ktk katiba yetu kwa namna nzuri ( ukiacha ubunge kwa hiari yako anateuliwa aliokuwa anakufuatia ktk kura za maoni) ili kuwazuia hawa wachumia tumbo
 
Nakuuliza mheshimiwa Spika ni kweli umeafiki uamuzi wa James Ole Millya wa kujiuzulu ubunge na uanachama wa CDM kwa niaba yake mwenyewe na kwa niaba ya wananchi wa Simanjiro? Yaani wananchi wa Simanjiro wamemtuma kufanya hayo kama vile hawajui ni kiasi gani cha fedha za mlipa kodi kinapotea kwa chaguzi zisizo na ulazima?
 
Sikinde ngoma waliimba ; nitamuuliza shemeji hapo nyumbani kuna kasoro gani,mbona watoto wamekimbia umebaki na wajukuu pia watasambaa jirekebishe waliosalia wasiondoke.
 
Katibu wetu yuko sahihi, watu wengi wanajua ushindi ni wetu CCM, so wengi wanakwenda kujiandikisha ili tu kupata kitambusho cha mpiga kura ili imsaidie ktk mambo mbalimbali ya kimaisha..!! Kwani kakosea nn?

Wameanza sasa wakati wa Magufuli kutaka vitambulisho kwa ajili mambo yao? Watu wamejua Magu hawezi siasa za ushindani na hana mvuto zaidi ya kutumia madaraka yake vibaya kutangaza wagombea wa chama chake.
 
Haya ndio Watu weusi ndio tunayoyaweza.

Ila jamaa nae aliondoka CCM kwa upepo hivyo sishangai kurudi huko.
Na hawa waliokuja na upepo wa lowasa ndio wakapewa nafasi huku wale waliokilea na kikipigania chama wakiachwa pembeni. Uongozi lazima ukiri kuwa kuna maeneo ulifanya makosa na unastahili lawama.
 
Waheshimiwa LOWASSA na SUMAYE hakikisheni mmemaliza kazi yenu vizuri kabla hamjarudi nyumbani,muda bado ,mpaka July 2019[/QUt
Tunachoomba Tundu lissu atakaporejea kukiinua chama tafadhalini muweke bunduki chini.tusilipuane marisasi tena
 
Mheshimiwa ungevumilia tu, hadi uchaguzi mwingine. Kuokoa kodi za wananchi zitazotumika kurudia uchaguzi
 
Mtu anaweza akawa Dr na bado akalia njaa
 

Ningefurahi sana kama mkuu angewambia kua wale wote ambao wanajiuzuru ubunge na kuhama chama, hakuna kufanya uchaguzi mpaka mwaka 2020, Hawa wanaojiuzuru wanatuingiza hasara, gharama kubwa ya mabilioni ambayo ingetumikakufanya mambo ya maana inagharamia uchaguzi amabao umesababishwa na maamuzi ya mtu mmoja aliye amua kujiuzuru....hii ni aina fulani ya ufisadi..
 
Sishangai yanayoendelea! anachokifanya ni kutetea tumbo lake na kuwaacha wananchi. Magu anasema hii ni serikali ya wanyonge tena walio wengi lakini ukweli utajulikana huko mbeleni na kuna tatizo kubwa ndani ya ccm ambalo wanalitengeneza wenyewe 2020 wataliona hili
 
Hawa Jamaa ni Pumbaf kabisa...kama wanania ya Kuunga Mkono si Waungie hukohuko kwao, au kwanini wasiondoke wote tu kwa pamoja kwenda huko wanakoenda na Tume ikafanya Uchaguzi Upya Mara moja ikaisha. Hizi CHEAP POLITRICKS zetu na Kutafuta Publicity zinazidi kutuumiza wananchi na Ipo siku tutachoka kuona Pesa zetu za Kodi tunazolipa kwa Kuminywa kila kona zinatumika vibaya na hapo ndio Mbeleko Itakapochanika na Watatuelewa tu Mbilinge letu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…