Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

Tetesi: Mbunge wa Simanjiro, James Ole Millya kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa

Francis12

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2016
Posts
7,533
Reaction score
22,281
Mbunge wa Simanjiro James Ole Millya,kuhamia Chama cha Mapinduzi muda wowote kuanzia sasa. Millya ni miongoni mwa wabunge wa Upinzani wenye ushawishi kanda ya kaskazini kutokana na uzoefu wa siasa za kanda hiyo.

======= Oktoba 7, 2018=========
Mbunge wa Simanjiro (Chadema), James Ole Millya amejiuzulu nafasi ya Ubunge na kujivua uanachama, amehamia Chama Cha Mapinduzi (CCM)
 
Hii biashara haiwasaidi lakini kwa aibu hawawezi kuiacha maana watachekwa (wataulizwa imeleta tija gani) hivyo watajitutumua tu kuendelea nayo kuliko ku-surrender.

Eti hawa ndio watu wa kuipeleka Tanzania kufikia katika uchumi wa kati!!

Wabongo mtasubiri sana!!
 
Huyu nilishamhisi na kumtaja siku nyingi. Washauri wa UKUTA wa Mererani. Aende zake, alisaidiwa alivyozidiwa na Ole Sendeka, sasa ameshiba! Kila la kheri kama anayo huo mpango tunaouhisi kwa matendo yake. Kama hana, utasamehe bure maana wenzake wametukera sana
 
kifo cha upinzani ni janga kwa watanzania wote. ndio maana yule mzee wa mwitongo alikubali kura 20% zishinde dhidi ya 80% kwa sababu maendeleo chanya yanaletwa nguvu mbili zinazokizana.
''AKITUMALIZA SISI ATAANZA NA NYIE'' TUNDU LISU
 
Back
Top Bottom