Ni wazi wengi wa hawa wanaohama hama sasa wanatambua kuwa hawataweza kugombea katika uchaguzi ujao kutokana na ile sheria iliyolitishwa na serikali ya kikaburu chini ya ccm ile ya kutimiza mwaka mmoja chamani. Je, hawataki tena kuwa wabunge? Ni wazi wanataka, ila hawaamini kuwa kaburu huyu ataruhusu uchaguzi wa huru na wa haki kwani mifano ya chaguzi ndogo na ule wa serikali za mitaa wanayo.
Kwa nini wanafanya haya ya kuhama? Ni wazi kuwa wanafahamu kuwa kaburu huyu haheshimu sheria au anaweza kutunga sheria nyingine ya kikaburu kuwapa favour hawa wahamaji au kuwakumbuka katika teuzi zake za UDC, uRAS na kila aina ya teuzi zinazoendelea kila uchao.