Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amjibu Spika Ndugai kuhusu kurudisha Posho

Mbunge wa Tarime Mjini, Esther Matiko amjibu Spika Ndugai kuhusu kurudisha Posho

Huyu bi mdashi Yuko vizuri na majibu yake yameeleweka, kumbe bado Yuko kwenye kituo Chake Cha kazi kwa Sasa.
Kituo cha kazi sio.mji alipo.MTU no ofisi.Kituo cha kazi wakati wote ni ofisini

Kituo cha kazi cha wabunge ni bungeni sio.mitaani.Iwe Dar au Dodoma.

Tafsiri ya Kituo cha kazi no ofisini sio nyamachoma au hotelini

Matiko kalamba milioni 110 kajifungia anazila peke yake tatatibuuu kajilock down kabisa asiombwe hela aisee ubunge mzuri ndio.masana katakata hasa milioni 110 sio.mzigo mdogo ndio.maana hadi akina sugu unakuta wanazidi kuwa wafupi tu ila wanafutuka hasa mpaka nashanga sugu mbona anazidi kuwa mfupi lakini anafutuka unene Huyo.hadi masikio kumbe kuna mzigo Wa Milioni 110 umeingia
 
Hakuna fani inayolipa kama ubunge katika nchi hii, yaani ukiwa mbunge kwa mm miaka mitano wewe ni moja wa watu wenye hali nzuri sana bongo. Ndio maana engineers, doctors, lawyers nk wameamua kuachana na fani zao wapo bungeni wakililia posho zao.

Ukitaka wabunge washikamane, ingilia maslahi yao, hapo utaona CCM na CDM kumbe ni chama kimoja.
 
Mkuu wabunge ndo wanaongoza kulipwa vizuri sana, hivi kweli kazi Moja MTU analipwa Mara 2 nni maana yake?
Ndiyo hivyo, watu wanatoboana macho kwenye kura za maoni huwa unafikiri ni nini Mkuu!!
jamaa wanakula

mzigo mkubwa sana huku wafanyakazi wengine wapo hali mbaya
Aisee nimeelewa kwa nini kila mtu anapambana awe mbunge awe ccm au upinzani. Inabidi wapunguziwe mishahara na posho.
 
Matiko acha kuwaiga kina Mdee na Bulaya watakupoteza

Wewe unaustaarabu jistukie utakufa kisiasa ukiendelea kuwaiga
Lakini mkuu huoni logic hapo?
Kama matiko anadai siku mbili kabla Ndasa kufa,alikuwa nae karibu,huoni logic Happ kwamba Ni vizuri aji isolate?.
Hata Kama Ni siasa ,this is too much bana,ushabiki wako umevuka mipaka,hata Kama unalipwa,ujue Basi na jinsi ya kukampeinia chama,maana unatutia aibu bana,,ccm hakunaga roho za kiikatili hivi,
Au haukupitia kivukoni front ukapikwa kisiasa,?
Ushabiki wako hauko kistrategy na huwezi kushawishi mtu yeyote maana Ni ushabiki uliojaa kiburi,majigambo na umbumbumbu
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Aisee nimeelewa kwa nini kila mtu anapambana awe mbunge awe ccm au upinzani. Inabidi wapunguziwe mishahara na posho.
true say man kwa huo mzigo lazima ujipendekeze mzigo mkubwa sana this world aint fair
 
Hakuna fani inayolipa kama ubunge katika nchi hii, yaani ukiwa mbunge kwa mm miaka mitano wewe ni moja wa watu wenye hali nzuri sana bongo. Ndio maana engineers, doctors, lawyers nk wameamua kuachana na fani zao wapo bungeni wakililia posho zao.

Ukitaka wabunge washikamane, ingilia maslahi yao, hapo utaona CCM na CDM kumbe ni chama kimoja.
nimegundua hakuna mwanasiasa mwenye uchungu na nchi wote ni maslahi tuu wacha wavuane nguo kwanzza ela zenyewe hatuzioni
 
Hakuna fani inayolipa kama ubunge katika nchi hii, yaani ukiwa mbunge kwa mm miaka mitano wewe ni moja wa watu wenye hali nzuri sana bongo. Ndio maana engineers, doctors, lawyers nk wameamua kuachana na fani zao wapo bungeni wakililia posho zao.

Ukitaka wabunge washikamane, ingilia maslahi yao, hapo utaona CCM na CDM kumbe ni chama kimoja.
Nimekuelewa sana mkuu. Huu ni ukweli.
 
Haya nenda Ufipa kuna nyumbu wengi km Wewe watakushughulikia
Hivi vijitu vingine sijui vimetokea wapi,kujifanya much know for nothing,,hakuna kitu vinajua kuhusu chama,vinaharibu taswira ya chama ,na havijali as long as kinaingiza buku saba
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Matiko tulimtoa pale UDSM kitengo cha Political Science and Sociology akiwa binti mdogo tena akiwa lecturer msaidizi. Tumemkuza kisiasa na kiimani. Nyie vilumumba uchwara mnakuzwa katika kuabudu na kutumikia tumbo. Wapumbavu wakubwa!
Toa boriti jichoni kwako kwanza
 
duuuuh kumbe wabunge wa upinzani wanazurumiwa pesa zao wanapohudhuria mahakamani? kwani pesa ambazo hawalipwi huwa zinaenda wapi? CAG amewahi kuzikagua?
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Chagua moja Mkuu aidha nilete mahari nikuoe au uende ukaolewe ufipa kuna nyumbu Wengi
Ha ha,hivi bia yetu una umri gani?,maana nisije kuwa naongea na mtoto wa miaka 17,form four failure,mtoto wa katibu kata aliepewa deal la kulipwa buku 7 kuropoka ropojka mitandaoni,
Nimekuwa nikisoma post zako nabaki kukuna kichwa tu,maana hujawahigi kuongea kitu Cha maana kikaeleweka yaani,
Kiufupi hauna qualification ya kukitetea chama chetu kitukufu,,haufai
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Hahaha Mkuu nipo tayari kukuoa, nipe location
Ha ha,hivi bia yetu una umri gani?,maana nisije kuwa naongea na mtoto wa miaka 17,form four failure,mtoto wa katibu kata aliepewa deal la kulipwa buku 7 kuropoka ropojka mitandaoni,
Nimekuwa nikisoma post zako nabaki kukuna kichwa tu,maana hujawahigi kuongea kitu Cha maana kikaeleweka yaani,
Kiufupi hauna qualification ya kukitetea chama chetu kitukufu,,haufai
 
ANAANDIKA MHE. ESTHER MATIKO (MB) AKIFAFANUA KWENYE KUNDI LA WHATSAPP LA TARIME ISHI NA MIMI

Bora ucheke Mdogo wangu..!
Hii nchi ni ya ajabu sana...! Juzi niliandika hapa posho zetu kama Michango nikaweka ( Perdiem 120,000/= n sitting 220,000/=) jumla 340,000/=. Maana hatuingii bungeni tupo karantini jamani pamoja Na kujichunguza afya..!

Mhe Spika anasema tumechukua posho...[emoji15]!

Posho ya kujikimu wanadai kutuwekea tarehe 1/5/2020 tukiwa karantini? Sijui Nini kipo nyuma ya pazia?

Kwa kawaida posho ya kujikimu huwa tunajaza form ndipo unaingiziwa kwenye account yako..! Na Tumekuwa tunafanya hivyo siku zote. Jana nimeshtuka kusikia eti kuna posho tumeingiziwa Maana sijaenda bank nipo karantini hapa Dodoma sitoki hata nje..! Kwa hiyo sijui kama kweli ama lah.

Kwa hiyo tumeingiziwa posho Za kujikimu bila kusaini? Upendo wa agape huu...! Ambao ghafla tulioingiziwa Fedha Za kujikimu bila kujua tunaitwa wezi? Hapa wanasheria waje watusaidie.

Turudi kwenye uhalisia. Let us assume Yaani tufanye wabunge wa Chadema walijaza form ya posho ya kujikimu( perdiem) Na kusaini labda tarehe 28/4/2020 kwa siku 16. Na hivyo siku 14 kuwa za karantini..! Sasa uhalali wa Mhe Spika kusema turudishe posho ya kujikimu unatoka wapi? Maana sio posho ya kikao kwamba umelipwa bila kuhudhulia?

Hii ni posho ambayo unalipwa kulipia hotel/ chakula n.k. Ukiwa kwenye kituo cha Kazi ambacho ni Dodoma. Sote Twajua matumizi ya perdiem..! Na wabunge wapo Dodoma kwenye karantini Lkn wanafanya majukumu yao mengine ya kibunge kwa njia ya mtandao sio lazima wawepo bungeni.

Kuna wabunge wengi sana wa CCM hujaza form Za hii posho siku ya kwanza Na kuondoka..! Je alishawataka kurudisha hizo Fedha tunawajuwa tena kwa majina. Ni dhahiri hajawahi Na hawezi kwakuwa hizi si posho Za kitako ( sitting allowance) bali ni posho ya ambayo hulipia Malazi Na chakula.

Niseme tu nimesikitika sana kwa hili , inaonekana kuna hidden agenda..! Probably more to come as he said it yesterday...!

Binafsi nafuata masharti ya matabibu ( wataalam wa afya)Najitenga na kujichunguza afya yangu. Marehemu Mhe Ndassa alikuwa Kaka yangu Na rafiki wa kweli kwangu , karibia kila siku nilikuwa naenda kwenye kiti jirani na kuteta naye hata siku Mbili kabla ya umauti wake. Hivyo lazima nijitenge kwa Muda.

Kwangu mimi afya yangu Na ya wale ninao wazunguka ni Muhimu sana kuliko hizo posho.! Kwa Miaka miwili tulikuwa kwa asilimia 80 tupo mhakamani wakati wa Bunge la bajeti sikuona walau hata barua ya Bunge ikiomba mahakama walau wazingatie vikao Vya Bunge Na kufanya kila baada ya siku 14 au mwezi..! Tuliweza poteza posho ya vika Zaidi ya siku 200 kwa wabunge Saba wa Chadema tuliokuwa Na kesi ( Mhe Mbowe, Mnyika, Heche, Mdee, Bulaya, Msigwa Na mimi). Ambapo posho Za vikao tu ni 220,000 * 200 ni 44,000,000/= (44ml).

Nilipelekwa gerezani kwa hilasiku 104 hapa napo nilikosa mamilioni ya shilingi, nilikosa fursa ya kuwawakilisha Wananchi wangu bungeni Na nje ya Bunge. Ijulikane tu nilifutiwa dhamana ambapo nilikuwa nimetumwa Na Bunge Kwenda Burundi , lakini sikuona Bunge wakinitetea ? Leo Nipo karantini kwa tahadhari huku nikiendelea na shughuli zangu Za uwakilishi shida ipo wapi? Maana gerezani ni total lockdown hamna hata mawasiliano.

Jana tu tulifanya kikao cha Kamati ya mfuko wa jimbo, ili kupitia bakaa ya 12.5ml ya tuliyopeleka kwenye Ujenzi wa Choo shule ya sekondari Tagota .

Tulifanya Teleconference na wajumbe na kufikia maamuzi kuwa Tshs. 2.5ml ziende kwenye manunuzi ya samani Za ofisi ya walimu ikiwemo partition ya ofisi. Maana nilipotembelea mwezi wa tatu . Nilikuta Walimu wote wapo kwenye darasa moja lilowazi hata Mwl Mkuu. Na Kilio kikubwa kilikuwa uboreshwaji wa Hiyo ofisi.

Hivyo hizi hisia hasi Na kuonekana tupo mikoani tunadhurula sio sahihi..!

Nasikitika tu kuwa hata tukiwa bungeni kwa ufinyu wa muda hatupati fursa ya kuchangia. Maana ya saa 4 tu Za kuwasilisha hotuba ya wizara, Kamati ya Bunge, hotuba ya upinzani , Michango ya wabunge, majibu ya mawaziri, hitimisho la Mtoa Hoja.......?[emoji848]

Hapa nakuachia wewe mwananchi uone kama wawakilishi wako tunakutendea haki. Unakuta upande wa Chadema wanapata watu wawili tu au mmoja wizara labda wagawane dakika tano .

Nilitarajia Bunge liende hadi July na Vikao vifanyike hadi Jumamosi. Maana tulipunguza masaa ya kikao kutoka saa nane kwa siku hadi saa 4 kwa siku .

Hivyo tungeweka wizara ya siku moja ya zamani kuwa siku 2, Na Za siku 2 kuwa siku 4. Lkn imekuwa kinyume ya wizara zilizokuwa Za siku 2( saa 16 sasa ni saa 4 siku 1, siku 3 saa 24 sasa Ni saa 4 siku 1 na ya siku 1 saa 8 zamani ni saa 4 siku 1 ya sasa. Bajeti Kuu ya serikali ilikuwa siku 6 saa 48 sasa Ni siku 2 Yaani saa 8[emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]

Nilidhani mngepiga kelele Bunge lisifupishwe ili wawakilishi wenu wajadili draft Za bajeti Za serikali kwa kina kuliko kinachofanyika sasa..’!

Huwa kila siku nashauri humu Tarime Ishi Na Mimi ..! Tuweke itikadi zetu pembeni, ili tuwe Huru kuchambua mambo kwa jicho la tatu. Bila kufanya hivyo tunaliangamiza taifa.

Wana CCM mnauwanja mpana sana kushauri kwenye vikao vyenu. Maana kwa sasa nyie ndo mmpewa ridhaa na wananchi, ya kukusanya kodi Na kupeleka maendeleo. Nawaomba sana mtambue jukumu lenu . Naona Mmekuwa mkikwepa majukumu yenu kwa kuitafutia Chadema ubaya...!

Tushikamane tuijenge Tarime Yetu.!

Mungu awabariki..!

Corona Ipo, Corona inauwa..! Tuchukue tahadhari.![emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji1431]

Esther Matiko (Mb)
Tarime Mjini.
Kumbe kuna pesa ndefu hv nje ya mshahara tukutane mjengoni #2030

Its not over until its over...[emoji769]
 
Back
Top Bottom