SI KWELI Mbunge wa Ulaya Valérie Hayer amepinga madai ya Lissu kuwekewa sumu

SI KWELI Mbunge wa Ulaya Valérie Hayer amepinga madai ya Lissu kuwekewa sumu

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Mbunge Hayer July 2025.jpg
 
Tunachokijua
Julai 2, 2025, Chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA) kilitoa taarifa kwa Umma iliyokuwa ikieleza kuwa kuna tetesi za kuwekewa sumu kwa mwenyekiti wa chama hicho Tundu Lissu ambyae kwa sasa yupo gereza la ukonga kwa mashtaka ya uhaini na kusambaza taarifa za uongo mtandaoni.

CHADEMA walipata taarifa hiyo kutoka kwa mbunge wa bunge la Ulaya David MacAllister ambaye alichapisha kupitia ukurasa wake wa X.

Valérie Hayer ni mwanasiasa kutokea Ufaransa ambaye ni mbunge wa bunge la Ulaya kuanzia 2019 kutokea upande wa wabunge kundi linalojulikana “Renew Erope” na amekuwa kiongozi wa kundi hilo kuanzia mwaka 2024.

Madai

Baadhi ya watumiaji wa mitandao tofauti ya kijamii ikiwemo X na Facebook kwa nyakati tofauti kuanzia Julai 03 walichapisha taarifa iliyokuwa ikieleza kuwa mbunge wa bunge la Ulaya Valérie Hayer amepinga kupitia ukurasa wake wa X, madai ya tetesi za Tundu Lissu ambayo yalitolewa na mbunge mwenzake.

Uhalisi wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji wa kimtandao kupitia utafutaji wa maneno muhimu, JamiiCheck imejiridhisha taarifa hiyo si ya kweli.

Picha ya skrini inayoonesha kuwa chapisho hilo limechapishwa na mbunge Hayer ni la kughushi kwani ufuatiliaji umebaini kuwa taarifa hiyo haikuchapishw ana Hayer katika ukurasa wake wa X.

Ufuatiliaji kwa njia ya mtandao kupitia utafutaji wa maneno muhimu hadi kufikia Julai 04, 2025 katika ukurasa rasmi wa mtandao wa X wa Hayer, hakuna taarifa yoyote ambayo ilitolewa na mbunge huyo ikiwa na jina la Lissu wala jina la Tanzania.​
Back
Top Bottom