TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

Baraka Mina

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2020
Posts
586
Reaction score
590
Mbunge wa viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa Ndg. Irene Ndyamkama amefariki dunia leo tarehe 24 Aprili 2022 katika hospitali ya Tumbi mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson ametangaza kifo hicho na kutuma salamu za pole kufuatia msiba huo.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Mwenyenzi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Tulia.

Mipango ya mazishi ya Ndg. Ndamkama inaratibiwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

IMG-20220424-WA0078.jpg


FB_IMG_1650806974019.jpg
 
Back
Top Bottom