TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

Alikuwa anasafr uchungu ukamshika njian maeneo ya kibaha akafanyiwa upstairs lakini ndo hivyo haikuwa ridhiki
Aisee Allah ampe kauli thabiti.

Binafsi huwa nikiona mjamzito huruma huniijia sana ukizingatia hali ya siku hizi vifo vipo jirani sana japo tunajifariji kuwa tumeendelea kwenye sekta hii.

Kwa sasa ukisikia mkeo/mpenzio nu mjamzito basi lazima uwe muangalifu kwa kila hatua, sisemi kwamba Mh. hakuwa na uangalifu ila nazungumzia jamii yetu kwa asilimia kubwa Mungu tuu ndio anayetusimamia.
 
Mbunge wa viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa Ndg. Irene Ndyamkama amefariki dunia leo tarehe 24 Aprili 2022 katika hospitali ya Tumbi mkoani Pwani alikokuwa akipatiwa matibabu.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Tulia Ackson ametangaza kifo hicho na kutuma salamu za pole kufuatia msiba huo.
“Nimepokea kwa masikitiko makubwa taarifa za kifo cha Mheshimiwa Irene Alex Ndyamkama, Natoa pole kwa familia ya marehemu, ndugu, jamaa, waheshimiwa wabunge na wananchi wa Mkoa wa Rukwa. Mwenyenzi Mungu awape moyo wa uvumilivu na subira katika kipindi hiki kigumu,” amesema Spika Tulia.

Mipango ya mazishi ya Ndg. Ndamkama inaratibiwa na Ofisi ya Bunge kwa kushirikiana na familia ya marehemu na taarifa zaidi zitaendelea kutolewa.

View attachment 2199028


View attachment 2199030

Poleni Sana. Inauma Sana.
 
Inna lillah waynailayh raj'un ameondoka bado binti mdogo sana. Apumzike pema Insha Allah !
 
Rest in peace Irene.

CCM Terrat tunatoa pole Kwa familia yake, wananchi wa Rukwa na Bunge na Tanzania Kwa kuondokewa na Mbunge huyu.
 
Kwenye Siri ya kifo ndipo mzungu kapigwa chenga na Mungu.
Poleni Sana.
 
Duh Maisha haya!! Alitumia nguvu nyingi hadi mtu jina la kihaya unawakilisha Sumbawanga!! Bado hajafaidi Matunda ya jitihada zake!! Na Mwenyezi amjalie pumziko jema!!
 
Ila nimesikia sio maramoja kwamba kwa suala la operation ya uzazi hapa Tumbi wanapewa vijana bila ya uangalizi wa madaktari.
Hata muda huu Kama mtakwenda pale wodi ya wazazi mtakutana na walioshonwa sivyo, waliopasuliwa sivyo wanaugulia pale.
Tusiandikie mate
 
Back
Top Bottom