TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

Kwa hii issue ya huyu mbunge tusisingizie madaktari, alipaswa kupumzika kwa kuwa alikuwa kwenye wiki chache kuelekea kujifungua na hata kwenye ndege walimzuia maana kwenye ndege kama una mimba zaidi ya wiki 34/35 hawakuruhusu kusafiri lakini pamoja na kumzuia lakini bado alisafiri kwa gari kutoka Dodoma. Inasikitisha kumpoteza Mtz mwenzetu (RIP) ila kupunguza mishemishe hasa safari zisizo na lazima wiki chache kabla ya kujifungua ni muhimu sana japokuwa mazoezi ni muhimu ila isiwe kwenye hali ya kujitesa.

Possibly amefika hospitali hali ikiwa mbaya maana uchungu umemkuta akiwa safarini, lakini pia inaweza ikawa hospitali zetu hizi kama ulivyosema
 
Ndo hivo rafiki yote yanawezekana kwenye nchi yetu, kikubwa sisi wenyewe tujitahidi sana kuepuka kujiweka kwenye mazingira hatarishi maana hospital zetu tunazijua wenyewe
 
Ndo hivo rafiki yote yanawezekana kwenye nchi yetu, kikubwa sisi wenyewe tujitahidi sana kuepuka kujiweka kwenye mazingira hatarishi maana hospital zetu tunazijua wenyewe
Ni kweli
 
Reactions: naa
Samahani sana kiongozi. Nadhani uandike vile ambavyo una uhakika navyo. Shida yetu ni kujifanya tunajua kila kitu. Haya uliyoongea ni upotoshaji mkubwa. Nikuhakikishie hakuna daktari au muuguzi duniani anayependa kusababisha kifo kwa binadamu mwingine. Vifo vingi vitokeavyo ni hama mazingira ya kazi si wezeshi na hivyo mtoa huduma anakuwa hana namna nyingine zaidi. Pili maneno kama yako haya ndio yanasababisha watu wengi kuchelew kutafuta huduma, hivyo kuwa katika hatari zaidi kwani inakuwa mgonjwa au mteja amefikishwa katika nafasi ambayo huwezi saidia. Tuwaachie wataalamu na tusionglee vitu ambavyo hatuvijui
 
Hili jina Ndyamukama utafikiri nila kule wanakolima kahawa na ndizi.
Au binti kaolewa huko?

Alikuwa binti yake wa Mbunge wa viti maalum mkoa wa Katavi Mama Lupembe! Mtoto alikuwa Viti maalum Rukwa, Mama Viti maalum Katavi! Hao ni Wabena ila huyu binti aliolewa na Muhaya! Walikuwaga na Hotel pale Mpanda ikiitwa enzi hizo Lake Tanganyika hotel na nyingine Sumbawanga ikiitwa White Inn hotel! Nadhani zote zimeshakufa sasa!
 
Mama wa marehemu nadhani ni mfipa anaitwa Lupembe kama sijakosea ni mbunge wa jimbo fulani huko Katavi.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app

Mama Lupembe siyo Mfipa ni Mbena aliyeweka maskani yake Mpanda. Pia yeye ni Mbunge wa viti Maum mkoa wa Katavi! Mama na mtoto wote walikuwa wabunge wa viti maalum kwa mikoa tofauti ya jirani!
 
Hii yaweza kuwa kweli mkuu,maana dada Irene tulikuwa naye arusha wiki hiyohiyo,alikuwa na mradi wake huko,na mume wake Mr Alex ndiye alikuwa akiusimamia,ila dada hakuwa mtu wa kutulia sehemu moja,alikuwa anasaka pesa kupita maelezo,watu wengi walikuwa wakimshauri atenge muda wa kupumzika,ila ndiyo vile alikuwa kwenye killed cha mafanikio na hakutaka fursa yoyote impite,Rip Irene tutaonana mbele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…