TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

TANZIA Mbunge wa Viti Maalum (CCM) mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamukama afariki dunia

Nilichanganya sio upstairs ni operation alifanyiwa tumbi alikuwa njian akitoka dom kwenda dsm sasa walipofika maeneo ya kibaha bahati mbaya chupa ikapusuka na siku zikiwa bado so huduma ya kwanza ni hapo tumbi ndo wakamfanyia operation mtoto akatoka akapelekwa muhimbili kwenye oxygen na hadi sasa yupo huko mtoto wa kiume ....na yeye pia alifanikiwa kuamka baada ya CS lakini mida ya jana alfajir hali ikabadilika akafariki mida ya saa 6 mchana
Pole nyingi sana. Huzuni kubwa mama kufariki wakati unamleta mtu duniani.

Na heri wangemkimbiza muhimbili na hali hiyo hiyo pengine wangeokoa maisha yake.

Wakati mwingine mimba zinasumbua sana.

Rest Easy my baby girl.
 
Akakutane na alie iba kura amweleze hali ikoje huku kwetu.
yaani Jitu likaanza kuwa-uwa wapemba alafu likakwiba kura nchi nzima isitoshe likamkufuru Mwenyezi Mungu, mwishowe likaoneshwa cha mtema kuni, za chini ya kapeti zinasema hata sehem ya kaburi lake ilipigwa na kuharibiwa na radi …………...
 
Aisee Allah ampe kauli thabiti.

Binafsi huwa nikiona mjamzito huruma huniijia sana ukizingatia hali ya siku hizi vifo vipo jirani sana japo tunajifariji kuwa tumeendelea kwenye sekta hii.

Kwa sasa ukisikia mkeo/mpenzio nu mjamzito basi lazima uwe muangalifu kwa kila hatua, sisemi kwamba Mh. hakuwa na uangalifu ila nazungumzia jamii yetu kwa asilimia kubwa Mungu tuu ndio anayetusimamia.
Mkuu nikuweke sawa: kifo kinachotokana na uzazi kwa mama mjamzito sio cha ghafla ...kinakuja kwa hatua, ambapo ni rahisi Sana kukizuia kwa kila hatua, yaani tangu mimba inatungwa hadi kujifungua pamoja na vitendea kazi duni na wahudumu wetu waliofuzu bila kuiva!
Swali linalonijia hapa ni je hadi mbunge anakufa kwa kifo kinachoweza kuzuilika kwa 95% tatizo liko wapi?

Namalizia kwa kukufuru! Wabunge mlipoamua kushiriki kuvuruga mitaala ya Afya mlidhani watakaoumia ni makabwera tu.
Afya ambayo vyuo vipo maghorofani, wanafunzi hadi wanapata vyeti huku hawajawahi kumuona mgojwa aliyeishiwa damu anafananaje, anatibiwaje, vyuo havina sehemu ya wanafunzi kujifunzia kwa vitendo kozi za miaka minne mkafupisha hadi miaka miwili mtu anahitimu!
 
Daah mama watoto wangu ni mjamzito miez 5 na alijifungua kwa Operation miaka miwili iliyopita nina mawazo sana aisee
Usiwe na wasiwasi... Anaweza akajifungua kawaida tu bila operation tena endapo sababu zilizopelekea kujifungua kwa operation mwanzo zilikuwa ni mtoto... Haikuwa kwa sababu ya maumbile ya mama...

Kama sababu ni mtoto... TAHADHARI JAMANI KWA WAJAWAZITO WOTE ESPECIALLY UJAUZITO WA KWANZA...

USIKURUPUKE KUMUWAHISHA MJAMZITO HOSPITALI PINDI TU UCHUNGU UKIANZA... MPAKA UJIHAKIKISHIE CHUPA IMEPASUKA... NA ANDAENI MAZINGIRA MAPEMA YA KUJIFUNGUA HATA AKIWA NJIANI ANAENDA HOSPITAL...

KOSA TUNALOLIFANYA WENGI... MKE ANAWAHI HOSPITAL UCHUNGU TU UNAPOANZA... UKIFIKA TU MOJA KWA MOJA THEATRE... HASA HOSPITAL ZA PRIVATE(Hapa maslah ya kipesa)... Hospital za serikali... Kama kuna wanafunzi ndio PRACTICAL SPECIMEN... AU UVIVU...

FACTOR NYINGINE... OPERATION ZIMEKUWA NYINGI HIVI SASA... ILI KUPUNGUZA RATE YA KUZALIANA(Uzazi wa mpango kwa lazima) ... COZ UZAZI WA OPERATION UNA LIMIT YA KUZAA...

USIMUWAHISHE MKEO HOSPITAL... LABDA ALIGUNDULIKA ANA KIFAFA CHA MIMBA AU PRESSURE YA MIMBA WAKATI WA CLINIC... KAMA ALIKUWA SALAMA TU... BASI WEWE MWACHE APAMBANE NA MAZOEZI MPAKA CHUPA IPASUKE NDIO MUENDE LABOUR...
 
yaani Jitu likaanza kuwa-uwa wapemba alafu likakwiba kura nchi nzima isitoshe likamkufuru Mwenyezi Mungu, mwishowe likaoneshwa cha mtema kuni, za chini ya kapeti zinasema hata sehem ya kaburi lake ilipigwa na kuharibiwa na radi …………...
Mkuu, hapa unayeumia ni wewe maana kwa maneno yako haya umebeba kinyongo na chuki kwa mtu ambaya wala hana habari kama kuna mtu anamchukia.

Naomba nikupe kisa kimoja cha mtawa wa kiume( au tumuite padre)
Sehemu flani kulikuwa na watawa ambao kwa Imani yao hawakuruhusiwa kukaribiana na wanawake. Siku moja watawa wanne walikuwa njiani kuelekea Kijiji jirani na njiani wakakuta mto umejaa maji huku akina mama wawili wakishindwa kuvuka kwenda upande wa pili na ndipo mtawa mmoja akawabeba wale wanawake mmoja mmoja na kuwavusha hadi upande wa pili, wale wanawake waliendelea na safari yao na watawa nao wakaelekea kule walipokuwa wanaenda.

Njiani mtawa mmoja akamuuliza yule mtawa aliyewabeba wale wanawake "hujui Imani yetu inatuzuia kuwakaribia wanawake na kwanini umediriki kuwabeba wale wanawake mgongoni kabisa?" Yule mtawa aliyewabeba wanawake akamjibu mwenzake hivi: "Mimi niliwabeba wale wanawake ila sasa hivi nimeisha watua chini, ila wewe nakuona bado umewabeba!"

Najua kichwa chako kitaelewa maana ya simulizii hili....
Endelea kumbeba JPM, endelea kumbeba simulizii za "uovu" wake ukiolishwa bila kutafakari"

Credit kwa mama D kwa kisa hiki cha watawa!
 
"Mimi niliwabeba wale wanawake ila sasa hivi nimeisha watua chini, ila wewe nakuona bado umewabeba!"

Najua kichwa chako kitaelewa maana ya simulizii hili....
Endelea kumbeba JPM, endelea kumbeba simulizii za "uovu" wake ukiolishwa bila kutafakari"
🙌
 
Mnatuonaga wendawazimu tunapopiga kelele hiyo wizara apewe kichaa kichaa wa kupambania huduma bora na kupunguza unnecessary loss of lives.

Mnaleta majungu ya kishamba kutetea watu wasio na uwezo kupewa wizara. Binafsi sijawahi muona Dr Gwajima na wala simjui as a person, ila nikisikiliza alivyokuwa anafanya troubleshooting kwenye ziara zake anauelewa mpana wa health services delivery; yaaani sana sana sana.

Ipo siku kuna watu humu mtajua system zenu za ulaji zikikata muanze kuishi maisha ya kawaida halafu muende kupewa huduma kwenye hizo hospitali nje ya muhimbili (ina afadhali tu sio bora vile vile) ndio mtatia akili.

Watanzania wanadhani kila kitu mzaha, wizara technical kama hiyo mnataka jitu lisilojua lolote kuhusu huduma bora na usimamizi wake ndio mnalilia awe waziri.

Tutaenda tu kwa namna moja au nyingine kukutana na hizo huduma mbovu wakati tupo vulnerable (kama huyu marehemu) na watu pekee wenye uwezo wa kukutoa salama ni medical professionals ambao wazembe. Kama utokutana na masahiba hayo wewe basi ndugu na jamaa wa karibu na kutoka ni bahati yote kwa sababu za high medical errors zenye minajili ya uzembe unaoepukika ambao atutaki mtaalamu aushugulikie kwa kubadili culture ya ufanyaji kazi wizara afya.
 
Hili jina Ndyamukama utafikiri nila kule wanakolima kahawa na ndizi.
Au binti kaolewa huko?
kura za maoni viti maalum ccm mkoa wa Rukwa huwa kuna rushwa za kila aina na za kiwango cha juu. Viongozi wa ccm mkoa na wilaya hawapendi wanawake wenye asili ya rukwa kuwa viti maalum....aliyebaki naye si wa rukwa ni wa asili ya Mbeya. Alikuwa amtumishi wa tanesco akajisogeza kwa wenye chama mkoa akawapa walichotaka nao wakampa alichotaka. Wamama wenye asili ya mkoa huo kila awamu wanapigwa chini hata majina yao yakichanua, kwa sababu hawatoi hupigwa chini.
 
Usiwe na wasiwasi... Anaweza akajifungua kawaida tu bila operation tena endapo sababu zilizopelekea kujifungua kwa operation mwanzo zilikuwa ni mtoto... Haikuwa kwa sababu ya maumbile ya mama...

Kama sababu ni mtoto... TAHADHARI JAMANI KWA WAJAWAZITO WOTE ESPECIALLY UJAUZITO WA KWANZA...

USIKURUPUKE KUMUWAHISHA MJAMZITO HOSPITALI PINDI TU UCHUNGU UKIANZA... MPAKA UJIHAKIKISHIE CHUPA IMEPASUKA... NA ANDAENI MAZINGIRA MAPEMA YA KUJIFUNGUA HATA AKIWA NJIANI ANAENDA HOSPITAL...

KOSA TUNALOLIFANYA WENGI... MKE ANAWAHI HOSPITAL UCHUNGU TU UNAPOANZA... UKIFIKA TU MOJA KWA MOJA THEATRE... HASA HOSPITAL ZA PRIVATE(Hapa maslah ya kipesa)... Hospital za serikali... Kama kuna wanafunzi ndio PRACTICAL SPECIMEN... AU UVIVU...

FACTOR NYINGINE... OPERATION ZIMEKUWA NYINGI HIVI SASA... ILI KUPUNGUZA RATE YA KUZALIANA(Uzazi wa mpango kwa lazima) ... COZ UZAZI WA OPERATION UNA LIMIT YA KUZAA...

USIMUWAHISHE MKEO HOSPITAL... LABDA ALIGUNDULIKA ANA KIFAFA CHA MIMBA AU PRESSURE YA MIMBA WAKATI WA CLINIC... KAMA ALIKUWA SALAMA TU... BASI WEWE MWACHE APAMBANE NA MAZOEZI MPAKA CHUPA IPASUKE NDIO MUENDE LABOUR...
What, the fck!!
 
Dah, Mungu ampumzishe salama. Kifo kinachotokana na uzazi kinauma sana jamani. Ameleta uhai(mtoto)halafu uhai wake unaondoka.
 
kura za maoni viti maalum ccm mkoa wa Rukwa huwa kuna rushwa za kila aina na za kiwango cha juu. Viongozi wa ccm mkoa na wilaya hawapendi wanawake wenye asili ya rukwa kuwa viti maalum....aliyebaki naye si wa rukwa ni mnyakyusa alikuw amtumishi wa tanesco akajisogeza kwa wenye chama mkoa akawapa walichotaka nao wakampa.
Mama wa marehemu nadhani ni mfipa anaitwa Lupembe kama sijakosea ni mbunge wa jimbo fulani huko Katavi.

Sent from my vivo 2015 using JamiiForums mobile app
 
kura za maoni viti maalum ccm mkoa wa Rukwa huwa kuna rushwa za kila aina na za kiwango cha juu. Viongozi wa ccm mkoa na wilaya hawapendi wanawake wenye asili ya rukwa kuwa viti maalum....aliyebaki naye si wa rukwa ni mnyakyusa alikuw amtumishi wa tanesco akajisogeza kwa wenye chama mkoa akawapa walichotaka nao wakampa.
Hicho alichowapa bado anacho mwenyewe. Imekula kwao.
 
Back
Top Bottom