PreGE2025 Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA: Ataka Rais Samia kuungwa mkono Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025

PreGE2025 Mbunge wa Viti Maalum CHADEMA: Ataka Rais Samia kuungwa mkono Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
3,141
Reaction score
7,205
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Salome Makamba amesema Rais Dkt Samia Suluhu Hassan anapaswa kuungwa mkono pindi atakapochukua fomu ya kugomea Urais katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 baada kukubali kutoa bilioni 6.7 kwaajili ya kujenga jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.

Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025

Kauli hiyo ameitoa katika Ziara ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya TAMISEMI iliyotembelea na kukagua ujenzi wa jengo hilo amesema Dkt Samia amedhamiria kuondoa tatizo la Vifo vya Mama na Mtoto katika Wilaya ya hiyo ambapo kwa Mujibu taarifa iliyosomwa na Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dk Baraka Msumi kwa siku Wanawake wanaojifungua kwa siku ni 20-25 ambapo kwa mwezi ni 600 .

 
Back
Top Bottom