Mbunge wa Viti Maalum UWT Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu amekabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Raja Sports Academy

Mbunge wa Viti Maalum UWT Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu amekabidhi vifaa vya michezo kwa vijana wa Raja Sports Academy

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Mbunge wa Viti Maalum (UWT) CCM Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu amekabidhi vifaa vya michezo (Mipira na Jezi) kwa vijana wa Raja Sports Academy iliyopo Kata ya Mtongani Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani.

Hawa Mchafu(Mb) katika ziara yake ameungana na timu ya Madiwani wa Viti Maalum wakicheza mpira dhidi ya Raja Sports Academy Katika Kata ya Mtongani Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani.

Hawa Mchafu (Mb) amepokea kero za Maji, umeme, Barabara na Kiwanja cha Michezo kwa Wananchi wa Kata ya Mtongani Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani na kuahidi kuzishughulikia.

Mhe. Hawa Mchafu (Mb) ameshauri Vijana wa Kata ya Mtongani Wilaya ya Kibaha Vijijini Mkoa wa Pwani kuwa Michezo ni Afya, Michezo ni Ajira, hivyo, watumie Vipaji vyao vizuri ili viwasaidie kujikwamua kiuchumi.

KATA YA MTONGANI WILAYA YA KIBAHA VIJIJINI MKOA WA PWANI

"HAKUNA KITAKACHOSIMAMA NDANI YA MKOA WA PWANI"
 

Attachments

Back
Top Bottom