Hali ya kisiasa ndani CHADEMA vs CCM mwezi Aprili 2021
Uimara wa chama dola CCM baada ya mwenyekiti mbabe aliyekuwa anaendesha chama kama jeshi la mtu mmoja kufariki upo mashakani.
Sasa kuna mgongano wa wazi ndani ya chama chenyewe cha CCM mara wasomi vs darasa la saba. CCM asilia vs CCM wakuja n.k
Katika vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa Tanzania kwa muda huu 2021, CCM ni chama dhaifu kupita vyote.
Kwa sasa, hata chama cha CHAUMA chini ya mwenyekiti mzee Hashim Rungwe ni chama thabiti kuliko CCM.
Muda huu CCM haina Mwenyekiti wa Taifa wala Katibu Mkuu wa chama, bila kusahau chama-dola cha CCM 'Mpya' kilizoea kuvinyanyasa vyombo vya dola lakini sasa vyombo hivyo vya dola vinasikia "kauli" tofauti tofauti toka kwa mwenyekiti Mpya mtarajiwa wa CCM na hivyo kuvifanya vyombo hivyo kujitafakari upya wajibu wake kwa taifa.
Kina Bashiru Ally Kakurwa, Humphrey Polepole na wengine wengi ndani ya CCM ina aina ya viongozi ambao viongozi walikuwa hawawezi kumuambia chochote Mwenyekiti ambacho wao wanaamini kinyume.
Na wana CCM kindakindaki kina Nape Nnauye , January Makamba na hata wazee kama Yusuf Makamba, Abdulrahman Kinana wameshaambiwa na rais wa awamu ya sita waikosoe vikali serikali iliyopo madarakani. Kauli hii inazidi kuichanganya kambi ya CCM wakuja waliozoea mapambio mwanzo mwisho ya kusifu na kutukuza.
Tukija katika dola, mwendazake aliiyumbisha na kuivuruga kabisa mfumo wa utumishi serikalini yaani civil service. Aliwachukua watu wasio na ujuzi wa utumishi serikalini na kuwapachika vyeo vya u DED, Makatibu Wakuu na kujaribu kuhitimisha pigo kuu la kuua utumishi serikalini kwa kumuapisha Dr. Bashiru Ally Kakurwa kama Katibu Mkuu Kiongozi ambaye ktk historia ndiye Katibu Mkuu aliyekuwa hana uzoefu kabisa ktk utumishi wa serikali kuu.
Tunaona serikali ya awamu ya sita imebaini mapungufu hayo inaanza kuwa shughulikia (purge) maDED waliobeba kwa ajili ya ukada wa CCM. Tayari tunasikia vilio vya maDED huko wilaya za Temeke, Bumbuli Lushoto, Simiyu n.k kuwa moto unawawakia ingawa waliibeba CCM oktoba 2020 ktk uchaguzi uliofanyiwa uchafuzi.
Tukija katika mhimili wa Mahakama tuliona Mwenyekiti mwendazaje RIP alivyouburuza na kuwapa vyeo vya ujaji kwa vigezo dhaifu mfano kuandika hukumu kwa kiSwahili huku kesi hiyo ikiwa ni nyepesi mno. Tayari muhimili huu unajipanga upya baada ya kusikia kauli zake mpya mheshimiwa rais wa awamu ya sita.
Bunge pia lilipelekeshwa kwa Spika kuelekezwa kuwashughulikia wabunge wake kwa kuwatoa nje ili waje kushughulikiwa na mwendazake nje ya Bunge. Wabunge wa CCM pia hawakuepuka kipigo cha kisiasa toka kwa mwendazake, ktk kuelekea uchaguzi wa 2020 walishughulikiwa na 'wajumbe' na kama waliweza kupenya walikutana na rungu la Mwenyekiti wa CCM.
Fastforward mwezi Aprili 2021 Wabunge wa chama dola wameanza kujipanga upyaa baada ya kutanabai ile mbeleko iliyowabeba kuwaingiza bungeni imetupwa na tunaona wanaaza kufunguka yale ya kweli ya majimboni mwao na ya mioyoni mwao.
Vyeo katika ngazi za uwaziri tumeona waliojiunga mwishoni ktk CCM toka vyama mbadala walitunikiwa vyeo huku wale waliokulia ktk UVCCM na Jumuiya za CCM toka utotoni wakiambulia kuwa backbenchers. Yote hii ilikuwa kuonesha CCM imekufa na sasa mtu mmoja ndiyo alikuwa kila kitu hivyo wasifurukute au kuwashwa kuhoji au kutoa mawazo mbadala. Hawa sasa matumbo yao yako moto kwani rais wa awamu ya sita hakubaliani na siasa za kuzinguana.
Swali kuu sasa 2021 April 27 ni kuwa je zoezi la kumtafuta Mwenyekiti wa Taifa CCM na Katibu Mkuu CCM litakwenda kwa utulivu mkubwa wa kisiasa ndani ya Halmashauri Kuu ya CCM NEC na Kamati Kuu yake na hatimaye chama kuibuka kuweza kuwadhibiti wanachama wake wote ikiwemo Mwenyekiti wao wa CCM.
Yetu ni masikio na macho mwisho wa mwezi huu Aprili 2021.