Mbunge wa zamani wa Ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na Spika Ndugai

Mbunge wa zamani wa Ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na Spika Ndugai

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
104,319
Reaction score
183,639
Mbunge wa zamani wa Ndanda, Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na mh Spika Ndugai naye ameitikia wito. Mwambe amesema ataukaribisha kwa moyo mweupe ushauri au uamuzi utakaotolewa na Spika wa bunge.

Amesema sasa anarejea rasmi bungeni kumalizia muda wake wa ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.

Akiwa Bungeni amesema atakaa upinzani karibu na Kiongozi Rasmi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anayetambulika kwa sasa ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mhe. Lwakatare.

"Nimefika Dodoma kama ambavyo nilisema, nimekutana na Mh Spika hivyo ninatakiwa kuendelea na shughuli zangu za Kibunge, mimi nitaendelea kuwa Mbunge wa CHADEMA na mchana huu nitahudhuria vikao vya Bunge, nilijiuzulu uanachama na nikaacha kila kitu hivyo Mh Spika amenitaka nimalizie kipindi kilichosalia" amesema Mbunge Mwambe.

Akizungumzia suala la kulipwa mishahara na posho zingine ilihali yeye si Mbunge, Mwambe amesema kuwa, "Mimi nasema kwamba Spika alikuwa halipi mshahara kwa Mbunge hewa, mimi nimelipwa mshahara wangu wa mwisho ni wa Februari 15, ambao nililipwa Machi na nilipewa nusu sababu ndiyo nilioufanyia kazi".

2391345_picmwambe.jpg
 
Wonders shall never cease..Me naona lengo ni kuzidi kuwapa hawa agenda ya kujadili kuwaweka busy.Wasiwe na agenda yao ya kuanzisha/kuendeleza.Mana haiingii akilini mtu alijitangaza tena hadharani kwamba nahama ,leo tena anakingiwa kifua
 
Mbunge wa zamani wa ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na mh Spika Ndugai naye ameitikia wito.

Mwambe amesema ataukaribisha kwa moyo mweupe ushauri au uamuzi utakaotolewa na Spika wa bunge.

Source: Mwananchi
Haya yanayotendeka bora mtu urudi kwenye ule usemi maarufu aliotuachia JAKAYA; "akili za kuambiwa, changanya na za kwako"

Cecil Mwambe umetoka mwenyewe CDM kwa hiari yako na kuhamia CCM, (picha zipo na voice clips). Hiyo posho ya Bunge unayoanza kuipokea leo ujue tayari ni mapatu haramu na ni uhujumu uchumi.

Tutakufuatilia namna utakavyoitumia, na utambue kuwa baada ya Magufuli kutoka madarakani utashtakiwa kwa makosa ya Anti Money Laundering.. Sisi ni wazalendo usijesema hatukukutonya. Ndugai atakuwa hayupo mida hiyo
 
Kweli kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Taarifa niliyoipata hivi punde inasema jamaa amesharudi bungeni rasmi, na atakaa upande ule wa KUB Rwakatare eti anaemtambua.

Taifa hili sijui tumelaaniwa au ni kitu gani.

But kuwa na CCM itself, naamini ni dhambi tosha inayostahili ubatizo wa maji mengi kuiondoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa ameivuruga sana CCM, atakayekuja kumpokea kijiti cha uwenyekiti atakuwa na wakati mgumu mno kukijenga upya chama hiki.

Mavuno ya haya yote yataonekana ndani ya muda mchache ujao, tuwe wavumilivu.
 
Taarifa niliyoipata hivi punde inasema jamaa amesharudi bungeni rasmi, na atakaa upande ule wa KUB Rwakatare eti anaemtambua.

Taifa hili sijui tumelaaniwa au ni kitu gani.

But kuwa na CCM itself, naamini ni dhambi tosha inayostahili ubatizo wa maji mengi kuiondoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ulitaka akae karibu na Esther Bulaya ili apigwe na Mdee!
 
Taarifa nilizozipata hivi punde zinasema Mbunge Davis Mwambe aliejiuzulu nafasi yake ya uwakilishi kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, ataendelea kuhudhuria vikao vya bunge kama kawaida.

Mbunge huyo alieitwa bungeni na Spika wa Bunge Mh. Ndugai leo, baada ya kikao cha muda mfupi na Spika, sasa atendelea kushiriki shughuli mbalimbali za kibunge mpaka pale ukomo wa bunge utakapowadia.

Atakaa upande wa kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ( KUB Rwakatare) anayedaiwa bado anamtambua Mh. Mwambe kama Mbunge halali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom