Mbunge wa zamani wa Ndanda, Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na mh Spika Ndugai naye ameitikia wito. Mwambe amesema ataukaribisha kwa moyo mweupe ushauri au uamuzi utakaotolewa na Spika wa bunge.
Amesema sasa anarejea rasmi bungeni kumalizia muda wake wa ubunge kwa kipindi kilichobaki
na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.
Akiwa Bungeni amesema atakaa upinzani karibu na Kiongozi Rasmi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anayetambulika kwa sasa ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mhe. Lwakatare.