Mbunge wa zamani wa Ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na Spika Ndugai

Mbunge wa zamani wa Ndanda Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na Spika Ndugai

Aisee hii maajabu nayo sisiemu inatuona sisi wapuuzi sana


It is never too late to begin. Start now
 
Vituko hivi unavipata Tanzania tu chini ya CCM
 
Mnapigwa kwa technicalities za kipuuzi kabisa, hakuna barua yoyote ofisini kwa spika ya huyo mtu kuhama chama hivyo ofisi bado inamtambua.
Maajabu ya dunia!Mwambe ana kadi ya uanachama ya CCM ila ni mbunge kupitia CDM!Shame!
 
Ofisi ya spika na bunge lake wanatumia vibaya kodi zetu, its time kuwapiga moja bila wakatulie na wajukuu zao kula pension zao. Wamechoka akili kabisa.
 
..Mwambe anatakiwa ajiongeze kama anachofanya ni halali kisheria na kimaadili.
 
Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM Darmpya Blog on Twitter
Hili nia ajabu la ngapi a dunia kwa NDUGAI?
 
Mbunge wa zamani wa Ndanda, Cecil Mwambe amesema ameitwa jijini Dodoma na mh Spika Ndugai naye ameitikia wito. Mwambe amesema ataukaribisha kwa moyo mweupe ushauri au uamuzi utakaotolewa na Spika wa bunge.

Amesema sasa anarejea rasmi bungeni kumalizia muda wake wa ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM.

Akiwa Bungeni amesema atakaa upinzani karibu na Kiongozi Rasmi wa Kambi ya Upinzani Bungeni anayetambulika kwa sasa ambaye ni Mbunge wa Bukoba Mjini Mhe. Lwakatare.

Hivi kwani lile rungu Ndugai alilompiga jamaa kichwani lilimrudia yeye kisogoni, ?

Lakini huyu Ndugai alishasema yeye mwenyewe asichezewe yeye ana file MILEMBE"

Nadhani Bunge la chama hiki linaendelea kuweka rekodi Ambazo shetani hata huko aliko anashangaa
 
71.-(1) A Member of Parliament shall cease to be Member of Parliament and shall vacate his seat......
(e) where a Member of Parliament ceases to be a member of the party to which he belonged when he was elected or appointed to be a Member of Parliament.

Nani anamtaalifu spika kwa maandishi kwamba mbunge amehama chama chake au amefukuzwa
(a) Mbunge mwenyewe
(b) Chama alichohama au kilichomfukuza
(c) Msajiri wa vyama
(d) Maneno ya kusikia mitandaoni

Kama yote hayakufanyika kwa nini hasirudi bungeni!
Sawa nenda kapige nyungu ulale. Umeshaingiza siku
 
Nchi hii kwa sasa haiendeshwi na katiba bali kwa matakwa ya rais. Hata akiamua mkewe leo awe mbunge wa 11 wa kuteuliwa watu wanashangilia tu.

Kikatiba huyu haliishapoteza sifa za kuwa mbunge lkn kwa kuwa katiba ndio hivyo tena haifuatwi ni amri tu za rais basi atakuwa mbunge.
 
Mbunge wa Ndanda kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Cecil Mwambe, amesema kuwa kwa sasa amerejea Bungeni rasmi kumalizia muda wake wa Ubunge kwa kipindi kilichobaki na kwamba yeye ni mwanachama halali wa CCM, hivyo uchaguzi ujao atagombea kupitia tiketi ya CCM Darmpya Blog on Twitter
Kwa maamuzi ya ovyo ovyo yaliyopo ktk mihimili yote, tena yenye baraka zote za wakuu wa mihimili hii mitatu, kuna kila haja ya kuwekwa kwa takwa la kikatiba kuangalia utimamu wa akili kwa wagombea na wateule wa nafasi za uongozi, hasa zile za kitaifa.

As a nation, we have turned to be laugh stock before the international societies. Kila siku hatuachi kuona kituko kipya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuuu nimemuona huyu Mbunge wa Ndanda akijaribu kutaka kukwepa mkono wa sheria huko mbele, amekuwa akijitetea kuwa yeye kweli sio Mbunge wa chadema ila ameitwa na spika ili aingie bungeni, ukiangalia ana hofu kuwa anachokitenda ni kosa la jinai, maaana anaenda kulipwa pesa ambazo ni za wananchi kinyume na sheria anahis kuwa huko mbele lazima yatakuja kumkuta tu.

Sasa anajaribu kupiga kele kele kuwa yeye hana kosa maana ameitwa, ujue hawa wanasiasa wanajidanganya Sana, mtu anadhani kuwa hali itakuwa hivyo miaka yote, hawajifunzi kwa lugemarila alichukua hela za umma kisa yuko na rais kikwete Leo hiii anacharazika huko, watu Walisema hizi hela ni za umma hakusikia had rais akajitokeza akasema sio za umma Lakini hawakujua kuwa huko mbele yanaweza kubadilika kiutawala Leo hiii anateseka had wale waliokuwa wakimpigia kelele wameanza kumuonea huruma kila kukicha.

Mwambe hajui sheria, yeye anaambia njooo anaenda anashindwa kutambua kuwa wanaomwita wanafanya hivyo ila kuwakomoa chadema, yeye anatumika ili kuwaumiza chadema, Wakati huo huo anajua kuwa hela anazoenda kulipwa ni kosa la jinai, huko mbele atakapokucha kukamatwa na kushtakiwa atakuja kusema kuwa yeye aliitwa akaitikia wito, swali moja tu kwa mwambe yeye akiambiwa kuwa uwa huyu mkate na panga ataitikia wito?

Atakuja kujibu kupokea hela Kama alivyokamatwa lugimarila na kushitakiwa kwa kupokea hela za umma na mwambe hivyo hivyo, ila ndugai nae atakuja kuitwa kwa kesi ya matumiz mabaya ya madaraka Kama mramba, wakuuu hawa wanasiasa hawasomi nyakati, huyu mwambe, na wote waliotangaza kuhama chadema Lakini wanaendelea kupokea hela za umma watakuja kuwajibika huko mbele maaana hata wao wanajua kuwa natenda makosa ya kijinai, walai huuu uongozi wa awama ya tano hautadumu miaka mingi nawaambia uongozi utarud kwa Ccm asili mtakuja niambia

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atafungwa miaka ya "future" ila siyo wakati huu tukiwa madarakani.
 
Binadamu ameumbwa na njaa lakini hii ya Cecil Mwambe ni kiboko.

Unaitangazia dunia kwamba umejiuzulu ubunge na kuhamia CCM tena umepokelewa na mjumbe wa kamati kuu na Sekretarieti ya CCM.

Kisha Spika anakutega nawe unategeka kirahisi kabisa kama kamdada ka standard six na chips za bodaboda!

Hakika Ufipa wangekupa Uenyekiti ungeuza chama.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom