Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
ZAYTUN SWAI AAHIDI KUTATUA CHANGAMOTO YA BWENI SHULE YA SEKONDARI YA MKONOO
Mbunge wa Viti Maalum CCM Mkoa wa Arusha Zaytun Swai, katika wiki ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani iliyoadhimishwa tarehe 08 Machi, 2023 alitembelea Shule ya Sekondari Mkonoo Kata ya Terat Arusha jiji na kuzungumza na watoto wa kike ambapo wanafunzi hao walipata nafasi ya kuongea na Mbunge kuhusu changamoto ya ujenzi wa bweni.
Zaytun Swai baada ya kuelezwa na wanafunzi hao kuhusu changamoto ya bweni, aliahidi kukaa pamoja na Madiwani wa Halmashauri na kuangalia namna watakayofanya ili kutatua changamoto ya ujenzi wa bweni kwa watoto wa kike.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Dada Mkuu wa Shule ya Sekondari Mkonoo, Namnyeke Zakayo alimshukuru Zaytun kwa kuwatembelea katika shule yao na kuwasikiliza. Pia, wamemshukuru kwa kuwapelekea miti 100 kwa ajili ya matunda na kivuli. Wanafunzi hao wamemuahidi kuitunza miti hiyo na kusoma kwa bidii.
Aidha, Zaytun alipata fursa ya kuhudhuria Maadhimisho hayo kama Mgeni Rasmi katika Chuo cha Uhasibu Arusha pamoja na Wafanyakazi na Wakufunzi wa Chuo hicho Ambapo waliandaa mafunzo mbalimbali, ikiwemo ya Ubunifu na Technolojia, Ukatili wa kijinsia pamoja na somo la kujitambua kama Wanawake!
Akiongea na wanawake wa Chuo hicho, Zatyun alisema, kila mmoja akisimama kwa weledi katika sehemu yake ya kazi, wanawake wataweza kumuunga mkono Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na hakuna mtu atakayejitokeza kusema wanawake hawawezi kufanya kazi.
Kauli Mbiu: Ubunifu na mabadiliko ya kitechnolojia, Chachu katika kuleta usawa wa jinsia!