Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MHE. ZAYTUN SWAI AITAKA SERIKALI KUONGEZA KASI YA KUPUNGUZA VIFO VYA WATOTO NJITI MKOA WA ARUSHA
"Je, Serikali ina mpango wa kupunguza vifo vya watoto wenye umri kati ya mwaka 0 - 1" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha
"Serikali kupitia Wizara ya Afya imeweka Mipango ya kupunguza vifo vya watoto wenye umri wa miaka 0-1 kwa kuongeza vituo vyenye vyumba Maalum kwaajili ya kutoa huduma kwa watoto wachanga wenye hali mahututi na kufikia idadi ya 175 mwaka 2023" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya
"Serikali inatoa mafunzo kwa watoa huduma juu ya namna ya kutoa huduma jumuishi kwa watoto wachanga na watoto wakubwa. Kuimarisha huduma za kinga na kuzuia magonjwa yanayozuilika kwa chanjo kama vile Surua, Nimonia, Kuharisha, Dondakoo, Kifadulo, Pepopunda na Polio kwa kuongeza utoaji wa chanjo za watoto chini ya mwaka mmoja kufikia kiwango cha asilimia 98 ya utoaji wa chanjo ya Pepo Pentthree" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya
"Serikali imeongeza vituo vinavyotoa huduma kwa watoto waliozaliwa wakiwa na uzito pungufu (Kangaroo Mother Care) ambapo kwa sasa vituo 72 na Hospitali 175 zinatoa huduma hizi. Aidha, mwaka 2023-2024 Serikali imepanga kuongeza vituo 100 ili kufikia vituo 347 ifikapo Juni 2024" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya
"Zaidi ya asilimia 70 ya vifo vya watoto chini ya miaka 5 vinatokea kati ya miaka 0 - 1, Je, Serikali haioni haja sasa ya kuweka mikakati mahususi na kuwekeza katika watoto wa umri huo" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha
"Hospitali nyingi za Wilaya Mkoani Arusha hazina mashine za kuwahifadhi watoto Njiti, Je, Serikali ni lini itapelekea vifaa hivi katika Wilaya zote za Mkoa wa Arusha?" - Mhe. Zaytun Seif Swai, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha
"Rais Samia eneo hili amefanya kazi kubwa sana kwa maana ya kuweka vifaa na mambo mengine. Tulikuwa na CT Scan 3 nchi nzima ila leo tuna CT Scan zaidi ya 50 nchi nzima. MRI 2 leo tuna zaidi ya MRI 19. Arusha vinakwenda kujengwa vituo 100 kwa watoto wanaozaliwa na uzito mdogo" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya
"Kuweka vifaa vya kusaidia watoto wanaozaliwa na uzito mdogo. Ukijenga vituo 100 pia na vifaa vyake vinawekwa ndani, kwahiyo tatizo linakwenda kutoka na hakutakuwa na hiyo shida tena" - Mhe. Dkt. Godwin Mollel, Naibu Waziri wa Afya