Stephano Mgendanyi
JF-Expert Member
- May 16, 2020
- 2,833
- 1,301
MBUNGE ZAYTUN SWAI ATIMIZA AHADI YAKE YA MILIONI 12.5 KWA UWT JIJI LA ARUSHA
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Arusha, Mhe. Zaytun Seif Swai ametoa Shilingi 12.5 kwa UWT Jiji la Arusha ikiwa ni ahadi yake aliyotoa kwa kutoa Shilingi Laki Tano (500,000) kwa kila Kata ya Mkoa wa Arusha kwaajili ya kuendeleza Jumuiya ya UWT.
Mbunge Zaytun Seif Swai amesema hayo katika Mkutano wa Majumuisho ya Ziara yake aliyofanya Arusha Mjini ikijumuisha viongozi kutoka ngazi za Matawi, Kata, Wilaya na hadi Mkoa.
Lengo la kufanya Mkutano ni kuwasilisha Majumuisho ya ziara; Kutekeleza Ahadi ya Shilingi Milioni 12.5 kwaajili ya kuendeleza shughuli za Jumuiya ya UWT Arusha Jiji
Aidha, Mhe. Zaytun Seif Swai amegawa Fimbo za kuwasaidia watu wenye ulemavu wa Macho. Amegawa Kadi 1,000 za Jumuiya ya UWT kwaajili ya kuongeza Wanachama wapya ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Jumuiya ya UWT
Vilevile, Mbunge Zaytun Seif Swai amegawa Sare kwenye kikundi cha Msanja kwaajili ya kuleta hamasa kwa wananchi kushiriki uchaguzi wa Serikali za Mitaa na Vitabu kwenye kila Kata vinavyoonesha utekelezaji wa kazi anazozifanya.
Mwisho, Mhe. Zaytun Seif Swai amemshukuru Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Mhe. Mrisho Mashaka Gambo kwa ushirikiano anaotoa kwa UWT na kuwachangia Shilingi Milioni Mbili (2,000,000) UWT Wilaya ya Arusha Mjini kwaajili ya Kuwezesha shughuli za Maendeleo ya Jumuiya.
Kazi iendelee!
Attachments
-
WhatsApp Video 2024-08-03 at 00.28.15.mp443.3 MB
-
WhatsApp Image 2024-08-03 at 00.29.49.jpeg90.7 KB · Views: 5 -
WhatsApp Image 2024-08-03 at 00.29.49(1).jpeg224.8 KB · Views: 6 -
Screenshot 2024-08-04 at 14-33-50 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png1 MB · Views: 7 -
Screenshot 2024-08-04 at 14-35-11 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png969.5 KB · Views: 7 -
WhatsApp Image 2024-08-03 at 00.29.51.jpeg264.4 KB · Views: 5 -
Screenshot 2024-08-04 at 14-35-24 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png918.4 KB · Views: 4 -
Screenshot 2024-08-04 at 14-34-40 Zaytun Swai (@zayswai) • Instagram photos and videos.png968.9 KB · Views: 5