Mbunge Zuena Bushiri CCM Viti Maalum Kilimanjaro ashindwa kujibu maswali ya Mkataba wa DP world na Serikali kwenye mkutano wa UWT

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Kuna kundi la Wabunge wanawake wanapita wakiitisha mikutano ya UWT kule Kilimanjaro.

Changamoto inayowapata ni kubwa na wanaonewa huruma.
Wanachapwa maswali na wanashindwa kujibu.

Kwa hali hii CCM ijitafakari na inatumie mbinu Chagua na nyingi ila kufanikiwa ni ziro.

Jana tarehe 30.7.2023 Akiwa Kata ya Karanga ,Moshi Mjini, Kilimanjaro Mbunge tajwa hapo Juu aliaibika baada ya kuulizwa maswali na akina mama kuwa :

1. Swali la kwanza : Kwanini mkataba umewabagua wenzetu wa zanzibar?

Jibu: DP world anazijua bandari Za Mombasa na Dar tu.

2. Swali la pili: Aliulizwa je huu ulio sainiwa na Rais na bunge ni mkataba au ni makubaliano?

Jibu: Ni mazungumzo tu.

Kwa hali hii, ninaishauri CCM ijitafakari kipindi cha ndiyo mzee kilishapita.

Baada ya kuona maswali yanamzidi nguvu alikimbia mkutano Akiwaacha wamama kikaoni bila kuwapa nauli ya kurudi makwao ila waliambulia soda moja moja fedha ambazo hazijulikani atazirejeshaje au alitumwa na nani.

Mbunge Zuena ameonyesha hana Hata uwezo wa kuwa mbunge licha ya kuzungumzia mkataba.

Hata lugha ya malkia iliyotumika kuandaa mkataba huo Mbunge Huyo ameshindwa kuisoma.

Ni aibu kwa Kweli.
 
Halafu hapo ni mboga kwa mboga tu! Huko ni KLM uelewa upo juu mind you
 
Mzanzibar yupo dubai

Dar es Salaam. Waziri wa Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Dk Ashatu Kijaji amesema kuwa bendera ya Tanzania kupandishwa kwenye jengo refu zaidi duniani la Burj Khalifa jijini Dubai ni zawadi kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Taifa.

Juzi, ilisambaa video kwenye mitandao ya kijamii ikionyesha bendera ya Tanzania ikiwa imefunika jengo hilo refu duniani lililopo Dubai.

Leo Jumatano Machi 2, 2022 Dk Kijaji wakati akizungumzia mafanikio ya ziara ya Rais Samia aliyoifanya katika nchi za Ufaransa, Ubelgiji na Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) amezungumzia suala hilo akisema hiyo ni moja ya mafanikio ya ziara hiyo.

Amesema kuwa bendera hiyo ambayo ilipandishwa kwenye jengo refu kuliko yote duniani ilipandishwa usiku wa kuamkia Jumanne ikiwa ni kuitangaza Tanzania na fursa zinazopatikana.

“Wote tumeona kilichotokea kule Jiji la Dubai, kuonyesha umuhimu wa ziara ya Rais aliyoifanya, ndani ya Jiji la Dubai walionyesha bendera ya Tanzania kwenye jengo kubwa zaidi duniani kama zawadi kwa Rais na Taifa letu’ amesema Dk Kijaji

Amesema kuwa siku moja baada ya kupandishwa bendera hiyo, usiku uliofuatia ilipandishwa tena pamoja na picha ya Rais Samia.

“Jana tena usiku wakarusha bendera ya Taifa letu ikiwa na picha ya Rais wetu hasa tukiwa kwenye mwezi huu wa tatu ambao tunasherekea malkia wa nguvu pote duniani na Tanzania tukiongozwa na malkia wa nguvu mama yetu Samia” amesema

Amesema kuwa hiyo moja ya njia ya kuonyesha na kutangaza fursa zinazopatikana Tanzania na kuwataka Watanzania kutarajia kuendelea kuona fursa zikiendelea kutangazwa kwenye jengo hilo.

“Katika kuendelea kuitangaza na kuuza fursa tulizonazo, Watanzania watarajie siku ya leo wataona pia bendera yetu ikiendelea kupandishwa kwenye jengo lilelile na leo hii tutakuwa na picha ya Mlima Kilimanjaro” amesema

Amesema hizo ni jitihada za kuitangaza Tanzania kwa wawekezaji kuwa nchi iko salama na ina fursa nyingi za uwekezaji na itafanyika kwa mwezi mzima.
 
Hii ni hadithi imekujaTanganyika baba anafariki wanawake wanauza Mali Za familia.
 
johnthebaptist njoo hukunuokoe jahazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…