Mbunifu wa bunduki aina ya AK 47, Mikhail Timofeyevich Kalashnikov

Mbunifu wa bunduki aina ya AK 47, Mikhail Timofeyevich Kalashnikov

Hiyo bunduki inapendwa coz risasi yake inaenda umbali mrefu km 2 na mita 160, Ni bunduki ya kivita raia haruhusiwi kumiliki.
 
Wangapi wamegoogle na wakaweza kutushirikisha kama ushiboy ??

Basi tu mkuu, kuna binadamu wengine wamezaliwa na hulka za kushangaza - wanapenda penda sana kuwaponda wenzao na kujifanya wao zaidi!! Yaana hawana habari kwamba kutumia search engines za mtandaoni ukapata habari/machapisho ya kusisimua, alafu na wewe ukawa na moyo wa kutafasiri na ku-share na members wenzako, hicho ni kipaji cha aina fulani - members wengi wamemshukuru USHIBOY kwa kazi nzuri, ni members wachache tu ndio wanataka kuwafanya wenzao as if hawajawahi kwenda shule!!
 
Pamoja na maelezo yote hayo bado hujui kwa nini AK 47 ni chaguo la magaidi? Pole sana.

ww unafikiri kwa nn maafande wa nchi za magharibi wanapenda bunduki tofauti na hiyo?
 
nchi zilizoendelea hawatumii sana bunduki yako uliyo sifia hapa


halafu mi naona ak47 inapendwa sababu ya bei yake, maana hata waasi wanazo nyingi inaonyesha ni bei nafuu. ak47 ingekuwa ni gari ingekuwa toyota VTs halafu hizo za magharibi zingekuwa range.

Hakuna vita inayopigwa popote duniani ak47 isihusike
 
Vip kuhusu dragnov.

Umenikumbusha mbali kuhusu dragnov,by the way nafikiri hii ni rifle kwa ajili ya kuua from a distant,ni maalum kwa ajili ya snipers. Dragnov haifai kwa mapambano ya ana kwa ana
 
U are my fact story teller. Thank u. Naipenda AK 47. Nimeiona pale Gaza strip. Nilikaa na Hamas mmoja aliibebelea kama mtoto na aliiheshimu sana.

Kuna mama mmoja pia mtaa mmoja nilikaa nae kama 3 days kila Usiku wakati wa kuwalaza wanawe 6, alipita vyumbani mwetu Huku kaibebelea AK 47 ndani ya vazi lake refu jeupe. Anadai ndiye mume wake wa pili baada ya baba watoto na wanawe 3 kuuawa!
 
Tupo hapa kujifunza mkuu.
Na kama wewe unapata access ya mtandao usidhani kwamba wote tupo Kama wewe.
By the way, jf hatutafuti sifa kijana.....
Umenena vema mkuu...mie nimeshtushwa na comment tata kama hiyo wakati Ushiboy kajitahidi sana kutiririka ki smart. ..
 
Hiyo Google haielezei kila kitu na siyo wote tunauwezo wa kutafsiri hiyo lugha kwa ufasaha

Mkuu mleta mada usife moyo toka kwa hao watoto wa mama kula kulala

Nifurahia mada ka hizi hasa hapa jf maana watu wanafunguka na tunapata kuongeza gb zetu
 
BUNDUKI MAARUFU IITWAYO AK 47

Luteni Jenerali Mikhail Timofeyevich Kalashnikov wa Urusi ndiye mgunduzi wa silaha maarufu sana katika uwanja wa mapambano duniani kote iitwayo AK 47. Ni bunduki iliyobuniwa na kutengenezwa na kamanda huyu wa Jeshi Jekundu (Red Army) la Muungano wa Kisovieti wa Urusi (USSR) wakati huo.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alizaliwa tarehe 10 Novemba 1919 eneo la Kurya, Altai, Urusi, ambalo kwa sasa linajulikana kama Altai Krai, Russia. Alijiunga na jeshi la Urusi mwaka 1938 na kupangiwa kama fundi wa vifaru na baadaye alipanda cheo na kuwa kamanda wa vifaru.

Mwezi Oktoba mwaka 1941 wakati wa Vita vya Pili vya Dunia, alijeruhiwa vibaya katika mapigano ya Bryansk na kulazwa hospitalini mpaka mwezi Aprili mwaka 1942. Akiwa hospitalini akitibiwa, aliwasikia askari wenzake wa Kirusi wakilalamikia udhaifu wa bunduki zao za Urusi katika uwanja wa mapambano. Baada ya kubaini udhaifu huo wa bunduki za Urusi, aliamua kutumia ubunifu wake kutengeneza bunduki bora zaidi za jeshi la nchi yake. Baada ya majaribio yake ya muda mrefu, hatimaye juhudi zake zilizaa matunda mwaka 1947 alipofanikiwa kutengeneza bunduki ya AK 47. Jina hili AK 47 ni kifupi cha maneno "Avtomat Kalashnikova model 1947"; namba 47 inasimama badala ya mwaka wa ugunduzi.

Luteni Jenerali MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV alifariki hospitalini tarehe 23 Desemba, 2013 akiwa na umri wa miaka 94 huko Izhevsk, mji mkuu wa jimbo la Udmurtia Urusi.
Huyo ndiye MIKHAIL TIMOFEYEVICH KALASHNIKOV, mgunduzi wa bunduki maarufu kwa jina la AK 47 ["Avtomat Kalashnikova model 1947


Mimi na wewe tutagundua nini? kupika kachori au visheti?
 
Hongera yake. Ila hawa wagunduzi wa silaha wana nafasi mbinguni??
 
Back
Top Bottom