Muulize lemutuz kuhusu mbuta nanga atakusimulia
- Well, jana nilisema na leo narudia tena ninamshukuru sana Mungu kwa kunisaidia akili ya kurudi nyumbani right on time na mimi at one point nilikuwa nimenasa kwenye mtego kama aliyomo huyu mama, na kuna wabongo wengi kama yeye wamekwama ila hawasemi mitandaoni sasa ndio wengine mjifunze kwamba mtu anapoondoka majuu kurudi home moja kwa moja kwa nini waliobaki wanamzushia majungu na matusi mengi sana ya ajabu kumbe kisa na mkasa ni hasira zao za kumuona mwenzao amejiondoa kwenye yale maisha ya jela bila kupenda.
- Wengi tulienda Majuu tukiamini kwamba kila kitu kule ni super baada ya kufika kule kama una akili kama zangu ndio unagundua huwezi kula maisha majuu mpaka uwe na elimu kubwa ndio maana nikaenda Shule, sasa huyu mama aliepelkwa na Mzungu mmoja aliyemuoa kule Moshi Milimani na kama kawaida ya Wazungu alipofika kwao ndugu zake wakamkataa kabisa huyu mama na hii inawakuta wabongo wengi sana, mzungu akajitahidi kuishi naye kwa siri lakini akashindwa na kumuacha ila akampa Uraia na cha kuanzia kwa hiyo huyu mama anaishi kwa malipo ya Serikali kwa wasiojiweza na wazee ni hela ndogo sana kwa hiyo msot of the times hana cha kufanya maana hana kazi ni kukaa home na kusubiri check mwisho wa mwezi, ndio maana ana muda mwingi wa kufanya anayoyafanya,
- Wazungu walitengeneza system yao ya maisha ili wanasheria na Madakitari tu ndio wale maisha, lakini kwa bahati mbaya sana wakatokea wasanii nao wakaingia kundi hilo la kula bata za kizungu ndio pamoja na kuepndwa sana wanawachukia sana pia wanapokamatwa kwa kutokulipa kodi huwa wananchi wanaowapenda wanafurahi sana inaitwa love and hate relationship, sasa wewe mbongo unakuja kwenye hiii system ya wazungu kama huyo mama darasa la Saba na umeletwa tu na mzungu, maisha ni magumu maana unakuwa jela bila kujua, kuishi kule maisha ni magumu maana ni limited hela wanayokupa ni ya chakula na rent basi imeisha, kurudi nyumbani huwezi unaogopa utaanzia wapi kuishi kule upo jela huna marafiki, huna maisha kwa ujumla sasa unakuwa frustrated kama huyu maama unaanza kufanya anayoyafanya,
- Hapa kuna wanaojaribu kumsifia eti anavuta visitors kwenye blog yake which is nonsense kwa sababu hana tangazo hata moja la biashara kwa sababu hakuna Kampuni inaweza kutangaza pale kwenye matusi kila kukicha na always kuwatukana watu usiowajua, yale machupi anayoyatangaza niambie anauza mangapi na kwa nani? Hata Wasanii wa bongo siku hizi wameshituka na umaarufu wa bila kutengeneza pesa wanaukataa kabisa, mtu mwenye akili timamu unatakiwa kutoa justification ya unachokifanya ili wenye akili wakuelewa unafanya nini, mimi simtukani mtu kwenye kazi zangu za mitandao lakini what ever I do nimefanikiwa kupata matangazo mengi na ya kampuni kubwa hapa nchini na nje na wananilipa mpaka nimeweza kuisajili na kuwa kampuni na nina ofisi gerezanni ya blog tu ambayo nimeajiri Vijana 3 siku hizi siigusi sana blog sasa kama hii justification haitoshi ya kazi zangu mitandaoni then niambie sababu ingine!!
- Sikatai ninamfahamu aliwahi kuja hapa bongo akakosa pa kufikia nikampa pa kulala nikamtembeza mjini nikampeleka mpaka kwenye Show ya Koffi nikamuingiza VIP nikawaomba Big Celebs wapige naye picha, siku moja akaomba kumuona Lady J dee nikampeleka tukaagiza chakula kikawa sio kizuri nikamwambia Gadner mume wa Jide akasema kiacheni msilipe kama vipi watupe kingine yeye akakataa kumbe amepiga picha kile chakula, aliporudi UK akaanza kumtukana Jide kuhusu kila chakula ndipo tulipoacchana njia panda since then ameamua kutengeza umaaurufu kwa kutumia jina langu na hasa kunitukana matusi mazito sana, lakini mimi binafsi hanisumbui ila namuonea huruma sana maana naujua mwisho wake ni mzee tayari hana mume aliwahi kutaka kumuiba mume kijana mmoja mbongo aliyekwua na mke wake akashindwa since then hakuna mbongo mwanaume anayemtaka, hana mtoto ndugu zake wapo huko kwao kijijini tu huku mjini hana ndugu kabisa ndio maana hajali anajua hakuna ndugu yake anaweza kuona anayoyafanya, seriously ana matatizo ambayo anatakiwa kusaidiwa hasa akiwa huko majuu lakini nani atamwambia maana ukimwambia tu atakutana blog yake na Insta mpaka mwisho wote wanamuogopa na wamemkimbia hana rafiki wa kweli ndio maana akipata mtu mmoja wa kuwa naye atapiga mapicha naye mengi kujionyesha kwamba ana marafiki,
- Ni sad story ambayo wabongo wengi mnaotaka kwenda Majuu bila mpango mnatakiwa kujifunza kwamba sio kila kinachong;aa ni dhahabu sio kweli kwamba Majuu ni kuzuri tu hamna shida no shida zipo na hii ni mojawapo ya mama mtumzima asiyejua la kufanya baada ya kuwa trapped kwenye system ya wazungu, soon watamchukua wanamhamishia kwenye nyumba za wazee na ndio zaidi maana atakuwa hana mtu wa kwenda kumuona, hana rafiki kama sasa alivyo, ndio mwisho wake na honestly kuna wabongo wengi sana huko majuu kama yeye, Wabongo kwenye mitandao wanatafuta entertainment kumbuka kwamba principle moja ya watumiaji wakubwa wa mitandao ni kwamba huwa hawana cha kufanya na naturally tunapenda negativity na udaku kwa hiyo mtu kama huyu mama lazima awe na followers wenye kufikiri kama yeye lakini wana akili kubwa ya kutooonyesha kwa jamii halafu ni mwanamke kwa hiyo always kuna gender sympathy kutoka kwa wanawake wengi so ni lazima wamsifie ingawa wanajua kabisa kwamba ni waste of time,
- Kwenye blog ukiweka habari za kufunguliwa Chuo Kikuu wataingia visitors 5 kwa 30 minutes ila ukisema Wema Sepetu hakulala usingizi jana usiku wataingia wabongo 100,000 kwa the same 30 minutes and then unakuta kuna wabongo wanaolilia maadili sasa huwa ninajiuliza ni nani hasa hawa kama sio wanafiki? Sasa kwa this kind of consumers sure ukiwa kama huyu mama utapata tu visitors ingawa sio wengi hana visitors wengi maana AIM hapa bongo wana dataz za blog zote za wabongo na namba ya visitors maana ni wao ndio wanawashauri makampuni makubwa nchini na nje wapi pwa kutangaza matangazo yao, ukienda pale ofisi zao karibu na Leaders Club watakuonyesha namba zote za blogs za wabongo ile blog haimo mimi ninaenda mara kwa mara pale kuhakikisha nafasi ya my blog, wale wanashauri makampuni kuwekeza kwenye blog 5 za juu, JF siku zote ni ya kwanza ninamshukuru Mungu blog yangu ni moja wapo kati ya 5 after only 2 years in the field,
- Anyways kwa kumaliza ninasema hivi wabongo hasa kina mama watuwazima huko UK wajitahidi kumsaidia huyu mama mwenzao kwa sababu kesi yake ni moja iliyojitokeza nyuma yake kuna kesi nyingi za namna hii wazungu wanaita Calling for help, maana binadam unapofikia kufanya mambo bila clear acceptable justifications kwa wenye akili ina maana moja kwamba una matatizo yanayohitaji solution, ni mtizamo wangu tu I cloud be wrong too!!
Le Mutuz