Mbuyu umeanguka: Ahmad Ahmad ashinda urais CAF, Issa Hayatou kwaheri mzee

Mbuyu umeanguka: Ahmad Ahmad ashinda urais CAF, Issa Hayatou kwaheri mzee

Issa Hayatou aangushwa urais wa CAF baada ya kushikilia nafasi hiyo kwa miaka 29! Amepigwa chini kwa kura 34 dhidi ya 20 alizopata kati ya 54 zilizopigwa. Mshindi ni Ahmad Ahmad rais wa shirikisho la soka la Madagascar.
 
Leo vitu viwili vimeifanya siku yangu kuwa nzuri, uamuzi wa mahakama dodoma kuhusu uchaguzi wa TLS na hii ya hayatou kupigwa Chini
 
Messi alikua na miezi tisa wakati huyu bwana anaingia madarakani CAF. Hayatou alitoka familia ya ki sultan huko Cameroon. alikua raisi wa shirikisho la mpira cameroon akiwa na miaka 28.
 
Afadhari!

Yule mzee uchu tu ulikuwa umemjaa huku akijua wazi hawez kuleta maendeleo yoyote zaid ya hapa tulipofikia
 
Kazi yake ilibaki kusinzia kwenye vikao lakini hakutaka kuondoka kwa heshima
 
Hayatou alishaanza mambo yetu ya Waafrika, angelikuwepo mzee wa kupindua matokeo kutoka visiwani nadhani tungeliongea mengine!
 
Kisiki cha mpingo cha ngoka naona yule raisi wa FIFA amefurahi sana.
 
Back
Top Bottom